Jinsi ya kupika ugali wa muhogo

Jinsi ya kupika ugali wa muhogo

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Hiki ni chakula cha asili ambacho kinaliwa kwenye jamii zetu..

Mahitaji
•Unga wa muhogo.

Jinsi ya kupika.
•Bandika sufuria yenye maji jikoni(kulingana na maitaji)
•Subiri mpaka maji yawe tayari kwa kupika ugali(yachemke 100°C)
•Tia unga wako kwenye sufuria na anza kusonga bila kuchelewa dakika 15 zinatosha.

Hapa kwenye kusonga ndio hutofautiana mapishi kulingana na aina ya unga,unga ambao mihogo yake iliyolowekwa nineona unasongwa kama dakika 5 alafu sufuria hutolewa jikoni kisha kuendelea kusongwa kwa dk 10 likiwa chini bila moto mpaka pale ugali utakapo lainika tayari kwa kuliwa.

Unga ambao mihogo yake haikulowekwa unaendelea kupikwa kwenye moto mpaka unaiva.

•Ipua ugali wako upo tayari.

NB.Hakikisha maji na unga vinaendana ukianza kupika usiongeze maji wala unga mpaka unaiva,lakini ikitokea ugali umelegea kwa kiwango cha maji kuwa mengi tia unga kidogo sana ili ukaze na ukitokea umekaza sana tia maji kidogo sana kuulainisha ukifanya makosa hapa utajikuta umekosea kupika.

Mboga ipi tamu unapendelea kula na ugali wa muhogo?
 
FB_IMG_15937926908278758.jpg
ukiupatia na samaki pia mtamu sana
FB_IMG_15937928726293368.jpg
Ugali wa muhogo mboga majani ya kunde na kunde zake.
FB_IMG_15937926258045167.jpg
😋😋😋😋😋mtamu sana kwenye kuku
 
Back
Top Bottom