Jinsi ya kupika vileja vya dengu

Jinsi ya kupika vileja vya dengu

Queen___

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
214
Reaction score
221
Habari wanaJf...
Upikaji wa vileja vya dengu

MAHITAJI
1.UNGA WA DENGU 3/4 KIKOMBE
2.UNGA WA NGANO KIKOMBE 1
3.VEGETABLE GEE AU SAMLI 1/2 KIKOMBE
4.SUKARI ILIYOSAGWA 3/4 KIKOMBE
5. HARUFU YA ROSE 1/4 KIJIKO CHA CHAI
6.BAKING POWDER 1/4 CHA CHAI
7.BAKING SODA 1/4 KIJIKO CHA CHAI.

JINSI YA KUPIKA
Changanya sukari na vegetable gee/samli kisha weka pembeni.
Changanya vitu vilivyobaki vizuri kisha changanya na mchanganyiko wako wa awali.
Tengeneza vidonge vidogo vidogo kisha bonyeza kidogo viwe flati ila visiwe vyembamba sana.
Choma kwa moto wa 180c kwa dakika 15-20. Waweza tumia jiko la mkaa pia hakikisha vinaiva vizuri.
Achavipoe ufurahie kwa kula au kuuza.
1470994997567.jpg


Asante....
-Queen Chagga.
 
Back
Top Bottom