Lagrange
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 2,365
- 2,732
Natumai wote ni wazima wa afya, wenye hali tofauti Mungu awajalie wepesi ,mrejee katika hali njema.
Niende moja kwa moja,,Maisha ni safari ndefu sana iliyo jaa milima na mabonde ,kuna wakati wa raha kuna wakati wa shida. Kuna watu hawabembelezi shida wanabembeleza raha tu. Tuko tofauti
Nikiwa mwaka wa kwanza chuoni miaka ya nyuma kidogo ,sikufanikiwa kupata ufadhali wa masomo ,niliishi maisha ya kuunga unga siku zijongee tu. Ada na michango mingine nilifanikiwa kulipa kwa wakati muafaka .Tatizo likawa ni fedha ya chakula kila siku nikiwa nalala hostel. Hostel hawaruhusu kupika kabisa. Maisha yalijongea hivo hivo kitabu tabu hadi nilipo kutana na huyu Mama (mwanafunzi mwenzangu)
Huyu Mama alikuwa anashida sana kwenye hesabu kidogo tofauti na mimi ,,kwa kuwa mimi nilikuwa nimepitia kidato cha sita na yeye alikuwa amepitia diploma ,nilikuwa msaada sana kwake kwenye hesabu za Integration ,differentiation, Probability na Liner programming
( Nilionywa sana kuuliza maswali magumu wahadhiri ,nilitamani siku moja kuuliza hesabu za Integration ,differentiation, ni za nini kwenye course ya "Business Mathematics" ila nilikaa kimya tu)
Tuendelee na Mada ,basi kutokana na njaa zangu niliona hii ni fursa kubwa sana ,maana kabla sijaanza kumfundisha huwa naulizwa Lagrange umekunywa chai? ,jibu langu siku zote huwa ni hapana ,na ilikuwa ni kweli sijanywa chai, basi ananunua chai kwanza ,ndo tunasoma.
Basi wakuu njaa ikiwa kali sana kipindi tunakaribia kufika kwenye mitihani ya semester ya kwanza mwaka wa kwanza ,Nikaunda mpango tuwe tunasoma mara mbili lengo langu ili niwe nakula kwa garama za Mama,kwa kuwa yule mama alikuwa amepanga nyumba nzima jirani tu na maeneo ya chuo akaniambia tutakuwa jioni tunasomea nyumbani kwake.
Kwa upande wangu niliona hiyo ni neema kubwa sana.Basi nikawa naenda kwake tunasoma nakula na kuondoka zangu.
Sitasahau siku tulisoma vizuri tu kitu kimoja kinaitwa "Lagrangian function" tuka solve maswali mpaka Mama akaelewa somo sana .
Baada ya hapo alikwenda chumbani kwake huko nami nikiwa sebuleni akaniita ,akaniambia njoo mwanangu .Nikamwambia nije wapi ! akanijibu "huku niliko" .Nikaona isiwe tabu nikaenda ,kuingia mule ndani (chumbani kwake) .Akaniambia nimsadie kusogeza tendegu la kitanda libane ukutani vyema na kabati la nguo likae upande mwingine.
Yule mama nilikuwa namheshimu sana sana ,nilivo ingia mule ndani alikuwa amejifunga mitandio ( tulivo kuwa sebuleni alikuwa amevaa nguo vizuri tu). Sikutoa eye attention sana nilifuata alichoniitia ,tulivo kuwa tunasaidia kuweka kitanda sawa tukahamia kwenye kabati ,sijui niseme kwa bahati mbaya au ni planned mission mitandio ya yule Mama ilidondoka chini ,alikuwa amevaa tu chupi basi (ya rangi nyeupe).
Wakuu nilitoka nduki sana chumbani kwa yule Mama ,nilihisi kama mwili umemwagiwa maji ya baridi .Kwenda kushika mlango wa sebuleni nitoke zangu njee ukawa umefungwa ,na yeye akawa ametoka zake chumbani amejifunga mtandio mmoja sasa Akaniuliza ,'unakimbia nini' ,' Akaniambia 'ukiwa na Mama ako usiwe muoga muoga, twende tukamalizie kazi nipike' nikagoma nikamwambia fungua mlango huu kwanza ,akachukua ufunguo aliko kuwa ameweka akafungua mlango nikaondoka zangu ,nikaenda lala bila kula maana niliweka matarajio ya kula kwa Mama.
Akanitumia SMS ,niswambie mtu yoyote kilicho tokea ,nikamjibu awe na aman ,hakuna mwanafunzi atakaye jua .
NB;;;Umasikini ni kitu kibaya sana .
Kama ulisha wahi ombwa ukasogeze kabati au kitanda karibu utupe kisa chako.