JINSI YA KUSAFISHA AKILI

JINSI YA KUSAFISHA AKILI

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
.

Karibu binti na mwana wa mama Afrika.

Ukiingia katika maandiko Subconscious Mind inaitwa moyo au roho.
Ukisikia fulani ana roho/moyo mzuri au mbaya ina maana hizo sifa zimejaa katika Subconscious mind yake.
Na ndiyo maana ya kauli ya Yesu kusema kimuingiacho mtu si najisi bali kimtokacho, ikiwa na maana chuki zikijaa katika Eneo hilo matendo yako yatakuwa ni chuki.

Subconscious mind ni ngumu kuitawala.
Kwa kujua hilo mabeberu Wanafanya kila namna kuichafua, Sababu watu wanaofikiri vyema ni tishio kwa utawala wenye mashaka.

Muumba aliufanya ufahamu huu kuwa mgumu kutawalika, sababu zipo nyingi ila moja wapo ni matendo ya lazima kimwili, kama kupiga mwayo, chafya, kupumua, pia ndiko hutoka nguvu za kufanya maajabu.
Ndiyo ufahamu unaoumba matukio ya maisha yetu. Hivyo asingeutenga ufahamu huu kwa mfumo aliouwekea tungekuwa kama maroboti au simu.

Tungekosa utashi kamili wa kiroho na kimwili hivyo kuna wakati ingetubidi kutoa baadhi ya viungo vya mwili vipate hewa, mwanga, au mtu akichoka ndiyo kachoka mpaka anakufa.

Usione unapiga mwayo, Chafya, umechoka, alafu unalala unaamka uchovu umeisha, ukazani ni matukio ya kawaida sana.
Hizo ni sehemu za kazi ya ufahamu huu, ili kurekebisha mwili uendelee kuwa vizuri.

Sababu ya Subconscious, hakuna uchawi wowote kwa madaktari katika kumfanya mtu kulala nusu kaputi na akaendelea kuishi.

Kuichafua hii part ni kuijazia mawazo yasiyo na faida kwako na kutokeza maamuzi yenye madhara kwako na jamii.
Ikiwa safi unakuwa na maamuzi mazuri yenye faida kwako na jamii nzima.
Ndiyo maana Mungu akaagiza,
"linda moyo wako kuliko vyote uvilindavyo".

Unalinda vipi? ni kuujaza mawazo mazuri na kuondoa mawazo mabaya.

Iwe ni katika maisha, ibada, elimu, sanaa na kila kitu hii njia itakusaidia kusafisha na kupakia mapya kwa muda mfupi.
Zipo njia nyingi lakini leo nakupa moja kubwa, rahisi na isiyo na gharama.

DAKIKA 60 KABLA YA KULALA.

Nitaanza na kuondoa mawazo/maisha usiyoyataka, ili uumbe maisha/mawazo unayoyataka.
Usione watu Maarufu, wanasiasa, viongozi katika kila nyanja, wasanii, ukadhani hayo mambo yanakuja tu kama zali, wanayaumba wenyewe, Ingawa si lazima iwe kwa muda mfupi zaidi.
Ndiyo maana wakasema Tabia uzaa mazowea.

Ili Subconscious ifanye kazi ni lazima unconscious iwe imelala.
Ndiyo maana ukiwa unaota ndoto mbaya, ni zao la mawazo mabaya.
Hata wanaoota yesu malaika, maria au Mungu humuunda kwa namna walivyowahi kufikiria Nje ya ndoto.

Muda rahisi wa kusafisha Subconscious ni dakika 60 hadi 30 kwa uchache kabla ya kulala.
Huo ni muda ambao mala nyingi, unachokifanya, kukifikiria, kukiona huchukuliwa na Subconscious na kuhifadhiwa, utake usitake.
Matokeo yake yanaweza kurudi katika ndoto au asubuhi ukaamka na hisia zinazoendana na tukio lilitokea usiku.
Sababu hata ukilala Subconscious inaendelea kufanya kazi.

Mfano unaweza ona video ya kuhuzunisha Kabla hujalala.
Ukaota tukio lenye kuhuzunisha ndotoni, au ukaamka Asubuhi yake ni mnyonge au mwenye huzuni, bila sababu.
Na hata unaweza jishangaa mbona nimeamka hivi.
Na wakati mwingine unaweza usijihisi hivyo ila mwingine akakuuliza, " vipi unaumwa, mbona huko hivyo?".
Utajibu upo sawa lakini Subconscious ilichukua tukio uliloliona jana na kulifanyia kazi na matokeo ndio hayo, wakati huo wewe umesha sahau habari ya video uliyoona jana au hata wakati fulani uliopita.

Kwa kuwa inaweza kubadili hasi kuwa chanya bila wewe kujua, basi tumia udhaifu huohuo ikubadilishie chanya kuwa na nguvu kiasi cha kuumba jambo unalolitaka.

Ukirejea kauli ya Yesu inayosema " Ukiwa na imani kidogo unaweza kuhamisha mlima.
Maana yake hipo hapa, kama ukiiwekea Subconscious jambo dogo tu na ikaamini inaweza kutokeza jambo au kitu kikubwa cha kidhahiri.

Kwa wanaovuta bangi hii part, huathirika moja kwa moja na matokeo yake.
Mvutaji hupelekwa moja kwa moja kwenye uhusika wa mawazo yake.
Anaweza kubeba peke yake, kitu kilichowashinda wanaume nane.
Anaweza kula na akamaliza chakula cha watu kumi na bado akalalamika njaa.

Anaweza kuwaza ni rais na anahutubia maelfu ya watu na mbele yake akawaona kabisa.
Ndiyo inayomfundisha muuaji namna ya kuuwa na kutoka eneo la tukio salama.

Hutokea hivyo sababu SubConscious inaweza kukutendesha kitu ambacho hakiwezekani, Ikakupa mbinu au majibu ya mambo unayoyafikiria sana.

Kama una simu unaweza rekodi sauti yako, ukisema vitu usivyo vitaka.
Mfano kama unapenda ulevi, unaweza jikaripia kuhusu jambo hilo na kisha utasikiliza ukiwa kitandani mpaka usingizi utakupitia.
Na kama una phone unaweza lala nayo kabisa. Kiasi ambacho unaweza ukaota mtu fulani anakukalipia juu ya hilo jambo.
Hata kama utaamka na kuona hakuna matokeo, endelea na utaratibu huo.
Matokeo ni kuanzia siku 21 hadi 30. Utajikuta umeacha/ umekuwa na fikra nyingine.
Kwa upande wa sanaa, Elimu, biashara, unaweza kufanya/ kufikilia kile unachokipenda dakika hizo kabla ya kulala au kujiuliza maswali tata ndani ya muda huo, unaweza fanya hivyo hadi usingizi ukuchukue.

Tuwe pamoja
 
Back
Top Bottom