Nakushauri usome maneno haya hapa chini, kuna maelekezo ya msingi kabisa katika Biblia
Warumi 12:17-21 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:``Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana. Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
katika experience ya maisha yangu nimeona hili likiwa suluhisho kubwa sana la wanaonikosea.
(1)Ninaanza kwa kumwomba Mungu msamaha pale yumkini kwa kujua au kutojua nimekuwa chanzo cha simtofahamu hiyo.
(2) Ninamwombea aliyenikosea msamaha kwa Mungu.
(3) Ninapingana na roho ya chuki kwa jina la Yesu kwenye maombi.
(4) Ninamwomba Mungu amfungue ufahamu ili ajue kuwa amenikosea.
(5) Naomba Mungu anioneshe ni wema gani ninaoweza kumfanyia ili kuushinda huu ubaya.
(6) Nachukua hatua ya kumfanyia wema(even if is costful),
(7) Nikipata neema naweza kuzungunza nae. Isiwe na mara tu mlipokosana, bali iwe baada ya muda fulani hivi ili kama kulikuwa na hasira zipoe kabisa.
UKWELI NI HUU: HUWEZI KUUSHINDA UBAYA KWA UBAYA AU KWA KUKIMBIA, USHINDE UBAYA KWA WEMA. HAKUNA UBAYA WOWOTE UNAOWEZA KUSTAHILI MBELE YA WEMA.