Rommy Ronny
JF-Expert Member
- Jun 16, 2015
- 664
- 884
Baada ya Kuona sehemu ya kwanza kitu gani kinasababisha kushindwa katika biashara ya network marketing, Leo tunaongelea sehemu ya pili kitu gani kinakuweza kukurudisha nyuma ushindwe kufanikiwa kupitia biashara hii.
1. USICHUKULIE KUKATALIWA KIBINAFSI
Watu wanaojiunga kwenye biashara hii lazima wafundishwe kwamba ukiambiwa hapana, Ahsante usiichukulie kama ndio umekataliwa ww. Mfano.
Mhudumu kwenye mgahawa anaweza ambiwa hapana ahsante na mmoja, ataambiwa sihitaji tena kwa sasa na mwengine anaweza pia ambiwa sipendi kahawa, Ila majibu haya yote hayamfanyi akakimbia akaenda chumba cha kubadilisha nguo na Kulia kwamba wateja wake wote wamemkataa. Na hiyo ndio ilivyo kama kwenye biashara hii kwa wafanya biashara wapya wanachukulia hapana kibinafsi, ila katika biashara yetu HAPANA yamaanisha kwamba muda wake sio sasa, na haimaanisha sikupendi wewe au nakuchukia unachofanya.
Katika biashara hii kukubali hapana ndio njia pekee ya kukutana na wote ambao watasema ndio. Kwahyo kwa njia hii zile hapana zote utazokutana nazo chukulia ni chanya kwamba muda utafika na hao watajiunga kwa team yako.
2.KUONGEA NA WATU WACHACHE KUHUSU BIASHARA
kama tutaongea na watu wachache kwa wiki kuhusu biashara hii asilimia ya kukataliwa ni kubwa. kumbuka hii sheria ongeza namba ya watu wakuongea nao kuhusu biashara na utapunguza asilimia ya kukataliwa.
Mfano unawajulisha watu wa 5 katika wiki unaandaa presentation uwafundishe, unawaambia kutakuwa na darasa nyumbani kwako jumamosi katika watu wa 5 wanatokea watu wawili na katika wawili hao unaowafundisha hamna hata mmoja anayejiunga unaanza wafikillia wale wa 3 kwanini hawajafika na kwasababu ulijiwekea kiwango cha watu wa 5 inakukatisha tamaa na kuona ni ngumu na unaacha biashara kati.
swala hili unaweza liondoa ukawa kwa wiki unawashirikisha japo watu 30 na katika hao 30 ukiandaa darasa wakaja watu 20 katika hao 20 kuna asilimia kubwa watu 10 wakajiunga na hapo utakuwa unafanikiwa na biashara yako kuendelea kukua.
Kwa leo naomba niishie hapa ila nitaendelea na sehemu ya 3 kuhusu hii biashara na kama tutaenda pamoja mpaka mwisho itakusaidia kukujenga na kufanikiwa.
Ahsanteni Sana
ROBERT MZIWANDA
E-MAIL: robertmziwanda@gmail.com