Rommy Ronny
JF-Expert Member
- Jun 16, 2015
- 664
- 884
Tunaendelea na Muendelezo wetu wa jinsi ya kushinda na uwe katika mafanikio katika biashara ya network marketing( Biashara ya Mtandao ) sehemu ya pili tulielezea sababu za kushindwa kufanikiwa kama Kuchukulia kukataliwa kibinafsi na Kuwasiliana na watu wachache ni baadhi ya sababu za kushindwa kufanikiwa na leo tunaendelea na muendelezo wa sababu zinazowafanya watu wengi kutofikia Malengo yao.
1. KUSIKILIZA WATU AMBAO HAWAJUI WANACHOKIONGELEA.
Ngoja nikupe mfano ni asili ya binadamu tunapokuwa na msisimko na kitu inaweza ikawa kinywaji kipya au Fursa ya biashara tunapenda washirikisha wengine, haijalishi kinywaji au fursa ya biashara tutataka kuwashirikisha watu hasa wale watu wa karibu sana na sisi, hiyo haina shida kama utawashirikisha ikiwa kama ni kinywaji ila kwa fursa ya biashara ya mtandao si sahihi mpaka uwe umefundishwa na una maarifa kuhusu biashara yao au kampuni yako, Kwanin? sababu kubwa na ya msingi inayofanya watu wasifanikiwe na wasifike mbali katika biashara hii ni ule msisimko wanaoupata wakijua kuna kiasi fulani cha hela mtu anaweza kupata na anapotoka katika presentation wanaenda moja moja kuwashirikisha ndugu, marafiki bila kuwa na idea hata kidogo ya jins ya kufanya hii biashara. Ni bora usiseme chochote kwa yeyote mpaka umefundishwa vizuri jinsi ya kufanikiwa katika hii biashara.
Utakapoanza ongea na ndugu na rafiki kuhusu hii biashara wataona umeanza kukata tamaa au umechanganikiwa na unafikilia kuanza biashara ya umachinga, japokuwa utadhani una ukweli wakila kitu jinsi ya kuongeza kipato kwa muda mchache bado Ndugu, Marafiki na Majirani hawajui kitu kuhusu hii biashara bado watakuona umechanganikiwa kwa kitu unachotaka kufanya.
Kutokana na hiyo sababu utakaposikia fursa usishirikishe watu wa karibu mpaka uhakikishe;
a) Umejiunga
b) Umeweka dhamira ya kufanikiwa katika biashara hii
c) Umefundishwa mbinu sahihi za kufanikiwa katika biashara hii
Kama bado hujavifanya hivyo tajwa juu usimshirikishe mtu au kumuelekeza mtu kuhusu hii biashara nasisitiza tena kama bado hujakamilika katika hivyo vilivyoorodheshwa juu usimshirikishe mtu zaid mualike kwenye madarasa ili afundishwe mpaka umeijua biashara yako.kama hujajiunga watajua bado hujaweka hela na haupo serious so watajitahid kukutolea mifano ya walioshindwa Mfano Unataka kufungua Mgahawa ukiwaambia ndugu, Marafiki na Majiran unataka kufungua Mgahawa japo hawajui hiyo biashara watakuambia wengi wamefungua hizo biashara na wamefunga hiyo biashara sio nzuri, ila kama utafungua Mgahawa na kuwaambia nimefungua Mgahawa watakuuliza wapi tuje tukuungisghe, so hakikisha umejiunga, umeweka dhamira na hii bishara ya mtandao na umefundishwa mbinu sahihi za kufanikiwa katika hii biashara. Kutokana na experience yangu katika hii biashara sababu kubwa ya kutofanikiwa katika hii biashara ni kusikiliza watu wasiojua wanachokiongelea.
2.KUTOSIKILIZA WATU WANAOJUA WANAONGEA NINI.( WALIOFANIKIWA NDANI YA BIASHARA)
Kwa mfano pale unapoamua kujiunga unaelekezwa kwamba msimfundishe mtu mpaka uwe nawewe umefundishwa vizuri upende kujisomea vitabu na kuangalia video na kusikiliza mikanda ya baadhi ya watu waliofanikiwa katika biashara ya mtandao ili ufanikiwe, na unafundishwa kama ujifunze kuongea na watu wengi kwa siku , usichukulie kukataliwa kibinafsi huyu ndio aliyekufany uingie katika biashara hii anakuelekeza haya. Hayo yote anayokuelekeza kwasabau ya experience yake katika biashara hii anajua kwanini anakuelekeza hivi, la wewe humsikilizi anachokuelekeza na unaamua kufanya mambo kwa unavyojua wewe matokeo yake unakutana na mitihani na kukataliwa na watu wakaribu na kuwasikiliza watu ambao hawajui wanaongea nini wanakuambia network business ngumu matokeo yake unaacha biashara na huendelei wala kufikia dhamira yako kwakuwa hukusikiliza watu wanaojua wanaongea nini kuhusu hii biashara.
Na Hapa ndio mwisho wa somo letu kwa leo. Tuendelee kushirikishana kuhusu biashara hii na kuona jinsi gani tunaweza ipuka na kufanikiwa katika biashara hii katika mwaka wa kwanza.
Kama unaswali au Ushauri au Maoni. wasiliana nami kwa
E-mail : robertmziwanda@gmail.com
contact : 0714054545