Jinsi ya kushinda na kufanikiwa katika network marketing (mwaka wa kwanza)

Jinsi ya kushinda na kufanikiwa katika network marketing (mwaka wa kwanza)

Rommy Ronny

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2015
Posts
664
Reaction score
884
Baada ya Kutofanikiwa kwa mara ya kwanza Katika Network Marketing( Biashara ya Mtandao ) Nilikaa na kujifunza na kusoma kutoka kwa waliofanikiwa ni jinsi gani naweza kuwa na kipato cha ziada kitakachonifanya niishi vizuri na kutimiza malengo yangu.

Kutokana na kujifunza huku kuhusu biashara ya mtandao nimeona leo nishirikishane na wenzangu ambao labda wanawaza jiunga na biashara hii au ambao wamejiunga tayari na wanafikilia au kuona wameshindwa au ambao wamekata tamaa, kuwapa Moyo na kujua vikwazo gani watakutana navyo mwaka wa kwanza wa biashara hii.
Mfano wa biashara za network marketing i.e Four corners alliance, Forever Living , Trevor , Edimark na zengnezo.

Leo nitazungumzia kuhusu KUKATALIWA ( PUUZA KUKATALIWA )

1. FANYA KUKATALIWA MSHIRIKA WAKO BADALA YA ADUI YAKO.

  • KUKATALIWA NA MUME/MKE
Kila mtu anakutana na kukataliwa na watu katika maisha ila kinachofanya kutuvunja moyo kabisa ni kukataliwa na watu wa karibu katika maisha tunaowapenda na kuwaheshimu na kutegemea kupata msaada toka kwao.kukataliwa huku na watu wakaribu husababbisha watu wengi kushindwa katika biashara ya mtandao kuliko sababu yoyote nyengine. Mfano halisi

Umetoka sikiliza biashara ya mtandao kila siku uliona haiwezekani ukaona waweza, ukaanza panga watu ambao utawasiliana nao na kuwa nao kwenye biashara hii kama timu yako. Unarudi nyumbani kutoka kwenye presentation ambayo umeelekezwa kuhusu biashara unarudi nyumbani ukiwa na shauku kubwa ya kumuelezea mke/mume wako jinsi gani mnaweza kuwa na kipato cha ziada so wamshirikisha, majibu yanakuwa hivi:
Mke/Mme: Hivi kweli unataka uanze fanya biashara ya kuuza products au kutafuta watu wajiunge kuanza kuwaomba watu hapana,kwanza hizi biashara ya mtandao nina rafiki zangu wameshindwa endelea na kazi yako ila hii biashara hapana.

Kwa majibu haya hasa kwa mtu wako wa karibu sana na unayempenda yatakufanya ushindwe kufanya biashara kama hujajiunga basi hata kabla hujajiunga au kama umejiunga basi utaishia hapo hata kujaribu kwamba unaweza fanikiwa.

NJIA SAHIHI YA KUZUIA KUKATALIWA NA MKE/MME
Kukataliwa na watu wakaribu yatokana na sponsor wengi kutowaeleza njia sahihi watu ambao wanataka kuwaunga au kuwapa njia mbadala ya kukabili hii njia ya kukataliwa, njia sahihi ilikuwa Sponsor kumuelekeza mfano Bob baada ya kutoka kusikiliza na kuelewa fursa ya kuhusu biashara ya mtandao na kutaka kujiunga sponsor angemuelekeza Bob kwamba kutokana na kutoijua biashara ya mtandao vizuri akifika nyumbani asimshirikishe mtu yoyote hata mkewe ila aandae siku nyengine ya presentation amchukue mkewe aende naye kwenye darasa akaelekezwe jinsi gani biashara ya mtandao inaweza wasaidia kufanikiwa katika maisha yao na wote waliofanikiwa kutokana na biashara ya mtandao, angefanya hivyo Bob asingekutana na kukataliwa na mtu wake wa karibu.

Mwisho wa sehemu ya kwanza.
Kutokana na leo ndio siku ya kwanza naanza kuandika kuhusu njia za kukwepa vikwazo vya kutofanikiwa katika biashara ya mtandao ( Network Marketing ) kwa mwaka wa kwanza, nisiwachoshe wasomaje wangu. Usikose sehemu ya pili tukiendelea kuelezea challenge ambazo zipo katika biashara ya network marketing na jins ya kuzishinda.

Ahsante kwa ushirikiano wako . Together we can.
Kwa mawasiliano na kama unamaswali au maoni tafadhali wasiliana nami.

E-mail : robertmziwanda@gmail.com
contact : 0714054545
4cornersalliance Member
https://www2.fourcornersalliancegroup.com/romeo15/join
 
Nimepita kwanza, badae badae kidogo.
 
Heheee
nimekuja haraka nikajua kunasomo hapa la maana kumbe ndio hivi? ndugu hio kitu hunidanganyi, kuna mdada mmoja alijiunga, tena kwa pesa ya kukopa, kaanza ushawishi miezi sita hajauza hata bizaa moja ya buku,kila anaemshawishi anamkwepa, watu wakaanza kumkwepa hata wasikutane nae akaamua kutupilia mbali bizaa na pesa aliyo toa, hii kitu watu hadi vijijini wanaijua ukijiunga hupati mtu,kwani wanajua ukijiunga anafaidika aliye kushawishi, ili nawe ufaidike mpaka ushawishi watu, pia gharama za kuuza bidhaa zao nikubwa, hahaaa uwiiii! huu ndo ukweli,
cha kufanya kula k.o.joa uka.lal.e..
 
Nashukuru bab d kwa comment yako nitafikia huko kwenye kuchukua mifano kwa walioshindwa na sio kuzungukwa na kusikiliza kwa walioweza na waliofanikiwa katka maisha jifunze kwa waliofanikiwa. Ndio maana natoa darasa kwa walioingia wakashindwa nin walitakiwa kufanya na wapi walikesha. Nimeongelea network marketing ila hyo mifano na nitakachokuwa naelezea approach hyo waweza tumia kwnye biashara yoyote na utafanikiwa.
 
Heheee
nimekuja haraka nikajua kunasomo hapa la maana kumbe ndio hivi? ndugu hio kitu hunidanganyi, kuna mdada mmoja alijiunga, tena kwa pesa ya kukopa, kaanza ushawishi miezi sita hajauza hata bizaa moja ya buku,kila anaemshawishi anamkwepa, watu wakaanza kumkwepa hata wasikutane nae akaamua kutupilia mbali bizaa na pesa aliyo toa, hii kitu watu hadi vijijini wanaijua ukijiunga hupati mtu,kwani wanajua ukijiunga anafaidika aliye kushawishi, ili nawe ufaidike mpaka ushawishi watu, pia gharama za kuuza bidhaa zao nikubwa, hahaaa uwiiii! huu ndo ukweli,
cha kufanya kula k.o.joa uka.lal.e..

Bab d kingne cjaongelea kuuza products cjaongelea kuhusu mtu kujiunga humo hzo ni mbinu sahihi kwa watu ambao wapo kwnye network marketing kwa mwaka wa kwanza wanatakiwa wafanyaje.
 
Back
Top Bottom