Jinsi ya kushiriki kwenye Mnada wa hatifungani za Serikali

Jinsi ya kushiriki kwenye Mnada wa hatifungani za Serikali

Mwakawasila

Member
Joined
Oct 23, 2024
Posts
23
Reaction score
20
1.Fungua akaunti ya uwekezaji (BOT CDS ): Ili kufungua akaunti hii mwekezaji anatakiwa aambatanishe vitu vifuatavyo.

a. Picha 3 za passport
b. Copy ya TIN certificate
c. Copy ya kitambulisho cha taifa

2.Baada ya kuhakikisha viambatanisho vinavyohitajika, mwekezaji anatakiwa Kujaza fomu ya kufungua akaunti ya uwekezaji.

3.Akaunti ikiwa imeshafunguliwa hatua inayofata, mwekezaji anabaini aina ya hatifungani anayotaka (miaka 2, 5, 7,10,15,20 na 25)

pamoja na tarehe ya mnada wa hatifungani iliyochaguliwa kupitia kalenda inayopatikana kwenye tovuti ya Benki kuu ya Tanzania (BOT)

4.Mwekezaji anatakiwa Kujaza bid application form ambayo ataiwasilisha ofisini Kwa wakala aliyemchagua kwenye soko la hisa na kusubiria matokeo ya mnada huo

5.Matokeo hutolewa jioni ya siku ya mnada ambayo hutokana na bei ambayo mwekezaji amejaza kwenye form,

mwekezaji anapaswa kufanya malipo siku ya kazi inayofuata. Ambayo malipo hayo hufanywa kupitia benki anayotumia muwekezaji.

6. Kiwango cha chini cha kuwekeza ni TZS millioni 1.

*Ikiwa unataka kuuza hatifungani ulionunua kabla haijafika ukomo wake(maturity), wasiliana WAKALA uliye mchagua kwa msaada Zaidi.

MWAKAWASILA
MWALIMU WA BIASHARA
UWEKEZAJI NA AFYA

Whatsap 0744980339
 
Asante mwalimu!

Tunaomba utufafanulie kwa urahisi maana wengine tunapata ugumu kuelewa kwenye page za websites za Bot, faida ya akaunti ya uwekezaji ambayo utapata ukiwekeza BOt na zinatofautiana kwa namna gani na UTT au hisa za masoko ya hisa.
 
Ikiwa unataka kuuza hatifungani ulionunua kabla haijafika ukomo wake(maturity), wasiliana WAKALA uliye mchagua kwa msaada Zaidi.🙏🏾
 
Asante mwalimu!
Tunaomba utufafanulie kwa urahisi maana wengine tunapata ugumu kuelewa kwenye page za websites za Bot, faida ya akaunti ya uwekezaji ambayo utapata ukiwekeza BOt na zinatofautiana kwa namna gani na UTT au hisa za masoko ya hisa.
Bond/HATIFUNGANI unaikopesha serikali na faida haibadiriki kipindi chote Cha mkataba

UTTAMIS ni mifuko inayokusanya wawekezaji tofauti pamoja na KUWEKEZA pesa zao kwenye BOND ZA SERIKALI NA HISA

HISA unamiliki kampuni Kwa kuchangia mtaji
 
Back
Top Bottom