Jinsi ya kustaafu na majengo ya kupangisha ukiwa kwenye Ajira/Biashara

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo, zipo njia tofauti tofauti ambazo mtu anaweza kuzitumia kutengeneza kipato endelevu kwa ajili ya kustaafu. Lakini njia ambayo ina matokeo bora sana ni ile ya kutumia nyumba za kupangisha.

Maana yangu ya kustaafu na majengo ya kupangisha.

Ni kufikia hali ya kuingiza kipato endelevu ambacho unategemea kitaweza kutatua changamoto zako za kila siku bila kutegemea kazi nyingine yoyote.

Hii haina maana kuwa umiliki nyumba za kupangisha na kuacha kazi zako za kila siku. Hivyo, nyumba za kupangisha zitakuwa ni njia pekee ya wewe kuhakikisha unajenga mfereji wa kipato endelevu.

Kwa kuwa lengo ni kupunguza makali changamoto za maisha za kifedha, unahitaji kulenga kwenye majengo ya hatari ndogo za kiuwekezaji. Majengo yenye hatari ndogo ni kama vile;-

✓ Majengo ya familia chache.

✓ Apatimenti ndogo.

✓ Hosteli ndogo.

✓ Fremu za biashara ndogondogo.

Majengo yenye hatari kubwa ya kiuwekezaji ni kama vile:

✓ Nyumba za starehe.

✓ Majengo na maeneo ya mapumziko.

✓ Majengo ya mikutano.

Mbali na kwamba kustaafu kwa nyumba za kupangisha kuna manufaa sana. Hata hivyo unahitaji kuchagua mbinu sahihi ya kuanza uwekezaji wako kutokana na sababu ya mtaji wako kushikiliwa kwenye nyumba yako ya kwanza.

Kwanini Majengo Ya Kupangisha?

Unapokuwa umeajiriwa unakuwa na muda mchache wa kujifunza, muda wa kuendesha biashara yako ya ardhi na nyumba na wakati huohuo unahitaji kwenda kazini ulikoajiriwa.

Majengo ya kupangisha humfanya mwekezaji kutengeneza kiasi kikubwa cha kipato endelevu cha kila wiki au mwezi bila kumlazimisha aache kazi yake.

Mbinu zingine (mfano; kununua na kuuza viwanja) utahitaji muda mwingi wa kujihusisha na biashara ya kununua na kuuza viwanja. Hatimaye utaona ajira ni kikwazo kwenye kukuza biashara ya ardhi.

Hapo ndipo inapoweza kuwa chanzo cha matatizo ya kupungua kwa jumla ya kipato chako kutoka kwenye kuuza viwanja.

Pia, majengo ya kupangisha huendelea kuingiza kipato endelevu miaka hadi miaka. Hivyo ukimiliki nyumba moja unakuwa umepiga hatua kubwa sana.

Hii ni kwa sababu unakuwa umepata chanzo cha mtaji fedha cha miaka yote kwa ajili ya kukuza uwekezaji wako huku ukiwa umeajiriwa.

Aina Ya Majengo Ya Kupangisha Kwa Waajiriwa.

MOJA.

Majengo ya kupangisha ya makazi ya familia chache.

Hapa kuna majengo ya familia moja, majengo ya familia mbili, majengo ya familia tatu na majengo ya familia nne.

Majengo haya yanapanda thamani kwa haraka mwaka hadi mwaka kulingana na hali ya uchumi mahalia wa mkoa au wilaya husika.

Majengo haya yanahitaji kiasi kidogo cha mtaji fedha. Majengo haya hayahitaji mwekezaji kuwa na uzoefu mkubwa wa uwekezaji.

Majengo haya huuzwa kwa urahisi na kwa haraka ukilinganisha na majengo ya familia nyingi na majengo makubwa ya biashara.

Majengo haya yana idadi kubwa sana ya wapangaji bora ukilinganisha na majengo ya familia nyingi na majengo makubwa ya biashara.

Kwa sifa hizi, ninawapendekezea waajiriwa kuanza na aina hii majengo ya kupangisha. Itakuwa rahisi kuhakikisha unatengeneza kipato chanya cha kila mwezi kwenye aina hii majengo.

MBILI.

Majengo ya biashara ya kupangisha.

Haya yanamhitaji mwekezaji au timu ya mwekezaji husika iwe na uzoefu na ujuzi mkubwa kwenye aina ya jengo wanalotaka kumiliki.

Mara chache, majengo ya aina hii yanakuwa na kipato kikubwa kuliko majengo ya kupangisha ya makazi ya familia.

Hivyo kwa hali nzuri ya masoko mahalia unaweza kuanza kuwekeza kwenye majengo ya biashara ya kupangisha ukiwa umeajiriwa.

TATU.

Majengo ya matumizi maalumu.

Haya hujumuisha majengo ya zahanati, vituo vya afya, kliniki za afya, hospitali, shule, vyuo, vyuo vikuu na kadhalika.

Majengo ya aina hii yanaweza kumfanya mwajiriwa atengeneze kiasi kikubwa cha kipato endelevu endapo ataingia mkataba wa miaka mingi.

Mwajiriwa ninakusihi kumiliki nyumba za kupangisha kwa ajili ya kujiongezea kipato endelevu cha kila mwezi mbali na mshahara wako.

Lakini sio lazima uwekeze kwenye majengo, unaweza kuwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji. Pia, unaweza kumiliki biashara kubwa.

Endapo unataka kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha ukiwa umeajiriwa karibu ujiunge na kundi la UWEKEZAJI MAJENGO. Ukiwa humu nitakuwa karibu na wewe hatua kwa hatua mpaka ufikie lengo lako.

Kama bado unasisitiza ni aina gani ya uwekezaji unakufaa. Fanya hivi, chukua notibuku yako nzuri hifadhi mawasiliano yangu.

Je, ni mbinu gani bora ya kustaafu kwa namna hi?.

Mbinu pekee kwa mazingira yetu ni ile ya B-R-R-R-R ya nyumba za kupangisha. Kwa mbinu hii yeyote aliye kwenye biashara au kwenye ajira anaweza kujenga kipato endelevu.

Muhimu; Nipigie simu kuuliza program ya ukocha ya KUSTAAFU NA NYUMBA ZA KUPANGISHA. Nipigie kupitia nambari ya simu ya +255 685 33 34 95.

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Daah maisha haya, Yaani unapanga uwekeze kwenye mijengo unajibanaaa afu mwisho wa siku una dead unayaacha!
 
uzi mzuri
 
Back
Top Bottom