Jinsi ya kutafuta eneo (location) kwaajili ya biashara

Jinsi ya kutafuta eneo (location) kwaajili ya biashara

Ibrahimeliza

Member
Joined
Nov 25, 2020
Posts
37
Reaction score
26
Watu wengi tushawahi kuwauliza watu eneo kwaajili ya kufanyia biashara fulani, yaani baada ya kupata wazo unalitekelezea wapi...??

Njia rahisi ya kupata eneo sahihi kwaajili ya biashara yako ni WAZO. Ndiyo wazo lako linathamani gani..?? Ukishakuwa nawazo fikiria wazo hilo au biashara hiyo ungependa kuwauzia watu wa aina gani....?? Sokoni..?? Maofisini...?? Wapita njia...?? Masikini...?? Wa saizi ya kati...?? Matajiri...?? Wanafunzi...? Wa vyuo...?? Shule ya msingi...?? Sekondari..?

Ukishajua bidhaa yako inastaili kununuliwa na watu wa aina gani kama wanafunzi au wapita njia, tafuta nenda katika mashule au barabarani au nenda eneo ambalo linawateja ulio walenga kuwauzia angalia eneo la karibu yao kama ni fremu au kibanda, kisha najua hautakuwa peke yako angalia wenzako wanauzaje ..?? Nenda kanunue kwao angalia madhaifu yao na ubunifu wao kisha utajua ufanyaje ili uweze kumudu ukianza biashara.

#-+×÷## Tatizo ni kwamba unaanza kuwa na wazo halafu ndotunatafuta eneo, kila eneo linafaa kwa biashara jifunze kwenda kwenye eneo fulani kisha jiulize unaweza kuanzisha biashara gani katika eneo hilo. Kuwa mbunifu.
 
Una hoja nzuri lakini uwasilishaji wake umeufinya sana!!!

Mfano hii line NANUKUU;Nenda kanunue kwao angalia madhaifu yao na ubunifu wao kisha utajua ufanyaje ili uweze kumudu ukianza biashara,hapa hujafafanua huyu atakaechukua hili wazo lako aende akanunue kwao hao waliopo eneo la tukio kisha afungue biashara kama wao ili awe mpinzani wao au?
 
Una hoja nzuri lakini uwasilishaji wake umeufinya sana!!!

Mfano hii line NAKUU;Nenda kanunue kwao angalia madhaifu yao na ubunifu wao kisha utajua ufanyaje ili uweze kumudu ukianza biashara,hapa hujafafanua huyu atakaechukua hili wazo lako aende akanunue kwao hao waliopo eneo la tukio kisha afungue biashara kama wao ili awe mpinzani wao au?
Kitu cha msingi hapa ni kujifunza na kuona wenzako wanafaje hata kaama utaanzisha hapohapo na kuwa mpinzani wao, hakuna ubaya katika biashara ndomaana azam akitua bidhaa fulani na Mo nae anatoa hakuna ubaya kuwa mpinzani.
 
Back
Top Bottom