Jinsi ya Kutambua ubaya wako kwa Jamii

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
WATU wengi huhangaika sana kujua kama wanaifurahisha jamii au wanaiudhi. Wengine wamefikia hatua ya kujiuliza, wamekosea nini watu wanaowazunguka mpaka wakajikuta wamechukiwa? Kisaikolojia fikra za namna hii, ni sawa na kutafuta gari kwenye mwanga kwa njia ya kupapasa!

“Nashanga mama mdogo ananichukia bure, tena hakuna kosa nililomfanyia lakini hanipendi tu” Je, wewe nawe umekuwa miongoni mwa watu wanaodhani unachukiwa bure?

Achana na hulka hiyo, hebu tambua ubaya wako kwa kuangalia vidokezo vifuatavyo, ambavyo naamini ukivisoma kwa umakini utagundua ni wapi unakosea hadi kufikia hatua ya kuchukiwa katika jamii.

Je, inapotokea umesababisha wenzako wajisikie vibaya huwa unajisikiaje moyoni mwako? Mfano ulikuwa katika mazungumzo ya kawaida na rafiki yako, lakini kwa sababu za kibinadamu akapokea mazungumzo yako vibaya na kufadhaika. Wewe unapotambua kuwa umemuondolea mwenzako furaha huwa unajisikiaje moyoni? Kama huumizwi na tukio hilo tambua kuwa wewe ni mtu mbaya.

Jiulize, katika maisha yako ni mara ngapi umewafanya wengine wafurahi kwa kuwatatulia matatizo yao, kuwasaidia wakati wa shida na kuwavusha kwenye hali ngumu za kimaisha? Au umekuwa mtu wa kusubiri usaidiwe hata kwa vitu unavyoweza kuwasaidia wenzako?

Tangu umeanza kazi umeshawahi kutoa sehemu ya mshahara/pato lako kuwasaidia wazazi na ndugu zako au umekuwa mtu wa kutoa visingizio vya hali ngumu ya maisha licha ya kuwa unafanya anasa mjini? Ikiwa hujawahi kuwasaidia watu kupata furaha, fahamu kuwa unaishi na ubaya kwenye jamii, jiandae kuchukiwa.

Je, unaposikia wenzako wana shida huwa unazichukuliaje?, je ni sehemu ya tatizo lako au hujiweka pembeni na kuwaachia binadamu wenzako wamalize matatizo yao? Ukiwa hivyo hicho ni kipimo kikubwa cha ubaya wako kwenye jamii unayoishi.

Umekuwa ukitumiaje uwezo wako wa mali au hata nguvu za mwili mbele ya wenzako? Je, ni kwa kuonea na kuwakandamiza watu uliowazidi? Ikiwa una tabia hiyo anza kujihesabu kuanzia leo kwamba wewe ni mtu mbaya mbele ya jamii.

Angalia mazungumzo yako, je yamekuwa ni ya kuwatia moyo watu, kuwafariji na kuwaelimisha au umekuwa mtu wa kutoa matamshi ya kudhalilisha, kuudhi na kuwavunjia heshima wenzako? Kama ulimi wako unatoa maneno yenye ‘sumu’ usitegemee kupendwa.

Je, umekuwa mtu wa haki, mwenye kuwatanguliza wenzako? Unaweza kutoa unachokitegemea ili kumsaidia binadamu mwenzio? Ukiwa huwezi kufanya hivyo na umekuwa mtu wa kukumbatia mali zako ujue wewe ni mbaya.

Toka ndani ya moyo wako unafurahia jamii kuwa na umoja au umekuwa mtu unayechochea migawanyiko baina ya watu wanaopendana? Endapo una tabia kama hiyo fahamu kuwa matendo yako ni mabaya.

Ni mara ngapi umezuia hasira zako kwa lengo la kuepusha migogoro? Unaweza kuvumilia kuonewa au umekuwa mtu wa kulipa kisasi kwa kudhamiria kufanya mambo mabaya kwa makusudi licha ya moyo wako kukuonya mara nyingi usifanye hivyo? Kama una tabia hiyo tambua kuwa huo ndiyo ubaya wako kwenye jamii.
 
Uko juu kaka,elimu tunayoipata humu JF ni darasa tosha hakuna haja ya kumtafuta mwalimu aje kufundisha maadili,mada zimechambuliwa vizuri na lugha nyepesi
 
unatuelimisha sana kwa hili na mengine niliyosoma, ila kwa hili inaonyesha kwamba ni syndrom imekuwa ikikutesa sana wakati fulani, Hii ni saikologia kwa hiyo nimegundua wwe mkuu MziziMkavu una au ulikuwa na shida hii,

sasa! kwa nini ulikuwa ukichukia watu wengine?

kwa nini ulikuwa unaghadhabika unaingiliwa katika mazungumzo au kitu chochote, kwa nini ulikuwa huna moyo wa kunyamaza na roho na nafsi yako vikiwa vimetulizana usubiri mlevi apite ili uendelee na hoja au mambo yako

kwa nn ulikuwa na au unapata hasira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…