Habari wakuu,
Naomba msaada jinsi gani naweza tengeneza website / blog ambayo itaweza kuonekana kwenye search engine ya Google
Ambaye anafahamu nipitie site ipi ili kutengeneza hiyo website / blog msaada tafadhari
Niwatakie majukumu mema ya kazi wakuu
Ranking up on Google and other search engine inachukua muda lazima blog yako iwe na content ambazo ni za kipekee. Pia isiyopungua miezi sita online.
Vile vile kama unataka kutengeneza leo kisha leo leo uwe rank up! kwenye search engine, Itatakiwa utoe pesa kununua traffic..
Ila kama una blog au website iko na siku zaidi ya miezi sita au mwaka na huonekani kwenye search engine.
Rekebisha SEO zako unazotegemea kuwa rank up! Maana kuna kitu kitakuwa hakiko sawa...
Pia kama una hata picha moja yenye copyright huwezi ku rank up!..
au kama una content uliyoicopy kwa website au blog nyingine bila kuformat uandishi wake ni changamoto.
Vile vile kama unatumia kingereza katika blog au website yako ku rank up sio kazi rahisi.. maana kuna competition ya kutosha hasa ukizingatia wengi wanakumia AI tools...
Hivyo unatakiwa kuwa unique as possible,
Vile vile kama ni self host ndoto ya ku rank up! Sahau...
Vile vile kama utahost web au blog yako katika hosting isiyo na nguvu ku rank up ni ndoto...
Mwisho wa yote unahitaji website ya namna gani?
Target traffic yako ni wapi?
Una masaa mangapi ya kuwekeza kwenye website au blog?
La mwisho japo sio muhimu una elimu gani ya web designing?
Na unataka utengeneze from scratch au read made theme/template/html
Rakims