Juice ya Tende-Maaana hii natengeneza mwenyewe nyumbani na pia shemeji yao hutengeneza kwa matumizi ya nyumbani
:-Mahitaji ni Tende na Maziwa
-Kwanza unaichambua Tende kwa kutoa Kokwa zake,na kubakia na nyama tupu
Kisha unaiweka kwenye blender na kuchanganya na maziwa kisha unaisaga na ulaini wake inategemea na unataka uwe vipi,ila bora zaidi kuwa laini Zaidi ili maziwe yachanganyike vizuri na Tendena ilete maana halisi ya Juice licha ya kwamba Juice ya Tende unatumia kijiko kuinywa,hahaha.
-Wingi wa Maziwa na Tende inategemea na unataka iwe na umajimaji kiasi gani kuna Juice ya tende nzito na Nyepesi.Juice ya Tende haitiwi maji kabisaa ni maziwa tuu
Mie hupendelea Zaidi nyepesi kiasi,maana ndio unapata fleva vizuri.
Ukimaliza hapo unaiweka kwenye jagi kisha unaweka kwenye fridge,ila hii ni hiari sio lazima,unaweza kunywa hivyo hivyo bila ubaridi na ipo vizuri tu.
Angalizo:Juice ya Tende haitiwi Sukari mkuu wala kitu chochote artificial
Karanga na Habat al Sawda(Habba Soda):
Hivi huwa tunaita kama vikorombwezo,kama vile chips,ni kwamba unaamua uweke salad au pilipili.
Sasa hivi vyote havichangaywi mwanzo,ila hivi hutumika pale tu unapotaka kuinywa.
Yaani unatia kwenye glass kisha ndio unaweka karanga au Habba Soda au vyote kwa pamoja
Karanga bora zaidi ni za kukaangaa,ndio zinanyambuka vizuri,maana unazisaga zinakuwa kama chenga chenga
Asije mtu akakuambia kwamba Unachanganya Karanga na Tende na Maziwa,hapo haifiki jioni Juice yoote itachacha.
Wakati Maziwa na Tende hadi wiki inafika ikiwa kwenye Uhalisia wake