Jinsi ya kutengeneza maziwa mtindi

Jinsi ya kutengeneza maziwa mtindi

MMOJA

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2012
Posts
445
Reaction score
259
Naomba msaada wana jf kwa anaefahamu jinsi ya kutengeneza maziwa mtindi na changamoto za biashara hii ili tuanze kufanya ujasiriamali huku pia. Thanks
 
Kutengenezaje mkuu? Maana ninavyofahamu mimi ni kuwa, maziwa fresh ukiyahifadhi sehemu ambayo haina baridi(jokofu), yanaganda yaani kuwa mtindi.
 
Ahsante mkuu, nashukuru kwa mchango wako, yani kiujumla nataka nijifunze kutengeneza kwa kuyahifadhi
 
ni pm nikuelekeze jinsi ya kugandisha maziwa mtindi alafu utaleta feedback kwa jf
 
ninavyojua unachukua maziwa fresh yaliyopoa kwenye chombo chenye mfuniko. Kisha unayawekea maziwa mtindi kidogo ili kuyaletea chachu. Unafunika na baada ya siku yanakuwa mtindi. Ili kuendeleza utakapotoa huu mtindi chombo bila kuosha unatia tena maziwa na yanapata chachu na kuganda.nimefanya hivi kwa kutumia mtindi asili sio hizi azam au asas. Anayejua kutengeneza cheese kienyeji please nimesahau.
 
Kwa manufaa ya wanajamii wote ingekuwa bora kama ugefunguka hapa sote tukanufaika na ujuzi wako, labda kama kuna malipo furani unayotaka toka kwa mwenye kuhitaji ujuzi toka kwako?????
 
ninavyojua unachukua maziwa fresh yaliyopoa kwenye chombo chenye mfuniko. Kisha unayawekea maziwa mtindi kidogo ili kuyaletea chachu. Unafunika na baada ya siku yanakuwa mtindi. Ili kuendeleza utakapotoa huu mtindi chombo bila kuosha unatia tena maziwa na yanapata chachu na kuganda.nimefanya hivi kwa kutumia mtindi asili sio hizi azam au asas. Anayejua kutengeneza cheese kienyeji please nimesahau.
ahsante Mama joe, pia kuna mwingine ameelekeza kua unayahifadhi hata bila kuyachemsha, so kipi ni bora kuyachemsha au kutoyachemsha!
 
ni pm nikuelekeze jinsi ya kugandisha maziwa mtindi alafu utaleta feedback kwa jf

Ahsante tarimo wa rombo,ingekua vizuri sana kama ungetiririka hapa ili wajisiriamali wote wa jf wapate kuongeza ujuzi na kunufaika
 
Kwa wale wanaofanya biashara kubwa, wanaogandisha maziwa mengi sana kama asas na wengineo wao hununua bacteria wa kugandisha maziwa ambao wanawaagiza kutoka nje.
 
ahsante Mama joe, pia kuna mwingine ameelekeza kua unayahifadhi hata bila kuyachemsha, so kipi ni bora kuyachemsha au kutoyachemsha!

inategemea wengi wanaofanya biashara mtindi hawachemshi. Lakini chachu ni lazima uweke, yale yaliyoganda bila chachu nafikiri huwa yameharibika na wengine huendesha pia yanaukali sio uchachu.
 
Kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa ni hatari kwa afya. Unaweza kupata magonjwa mengi ikiwepo TB na magonjwa mengi kutoka kwa ng'ombe aliyeathirika. Nivizuri ukachemsha maziwa kwanza kabla ya kunywa au kugandisha. Usinywe maziwa mtindi yaliyogandishwa kienyeji bila kujua hali ya usafi wa aliye gandisha, ikiwepo kuchemsha.
 
watu hawaelewi na hubishia kuwa ile kuchacha huua vidudu. Vyakula mtaani ni hatari
 
huo uchachu unautoa wapi au unapatikanaje ili mtu aweze kua nao awe anaweka kwenye maziwa yanayotaka kuganda?
 
unaweza nunua kwa wenye hoteli au wauza maziwa au wafugaji ni mara moja tu. Baada ya hapo chombo ulichogandishia huoshi unaweka maziwa yaliyopoa yanaganda mradi uwe msafi na kuvifunika vizuri
 
Naomba msaada wana jf kwa anaefahamu jinsi ya kutengeneza maziwa mtindi na changamoto za biashara hii ili tuanze kufanya ujasiriamali huku pia. Thanks

Mkuu kama unaweza pata contact ya sua pale kuna wataalam wanatengeneza mtindi mzuri sana na kwa hali ya usafi, nafuatilia pia na nikiipata nitaiweka hapa
 
Ahsante kwa ushauri mkuu, tupo pamoja
 
Back
Top Bottom