Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

bro u a beast!!!
 
hivi unaweza kukata tumbo kwa mazoezi bila kuacha misosi kama wali na ugali ????
 
Kamanda eti pili pili ina madhara kwenye mazoezi?
Maana baadhi wanasema inakata pumzi!!!
Ndimu je?
Mimi situmii pilipili kabisa hivyo hili siwezi kukuthibitishia ila ndimu haina ubaya kwangu ndiyo juisi ya haraka niliyokua nakunywa nikimaliza mazoezi.

Ila hata kuhusu pilipili naamini ni stori tu.
 
Umeongea ukweli mkuu.
Ila Tukiachilia mbali swala la genetics kwa baadhi ya watu, wengi wetu tukila balanced diet ni kunenepa na mwisho kujipa kitambi.
Hapo ndipo shida ilipo sie wengine tukila mboga mboga mwili unakaa vyema ila ukileta mambo ya balance diet ndambi hilo!!
je maini ya ngombe hayana madhara?
 
Hapo ndipo shida ilipo sie wengine tukila mboga mboga mwili unakaa vyema ila ukileta mambo ya balance diet ndambi hilo!!
je maini ya ngombe hayana madhara?
Unafanya mazoezi kwa mtindo gani? Casual au hardcore?
 
Kuna article moja ilionesha kua kufanya mazoezi jioni ni vizuri zaidi kushinda asubuhi.
Binafsi ninaweza kufanya mazoezi kabla ya kulala.
Unafanya kabla the au baada ya chakula cha usiku?
Je Yafaa kufanya ukiwa umeshashiba?
 
Unafanya kabla the au baada ya chakula cha usiku?
Je Yafaa kufanya ukiwa umeshashiba?
Sijawahi kufanya mazoezi nikiwa nimeshiba kwakua kipindi naingia gym muda wangu ulikua ni saa 12 alfajiri mpaka saa 3 au saa 10 jioni mpaka saa 1.

Hiyo siyo mida ambayo nakua nimeshiba.
 
Unafanya mazoezi kwa mtindo gani? Casual au hardcore?
Naweza sema ni beginner Nakimbia Jogging dakika 30, push up za kawaida 20*3, sit up nikiwa nimezuia miguu kwenye tofali 50, leg raises *50, flute kick *50.'
Nataka ondoa Kifriji na kupunguza mwili plus 6Pack shida huku JNHPP Msosi ni wali /ugali nyama+harage kila siku.
Asubuhi naskip maana ni mikato na viazi vitamu....
Ushauri please hakuna chaguo hata vya kununua kuna chapati na vitumbua tu
 
Ukifuatilia page ya tatu au ya nne utakuta kuna watu wamequote uzi orijino kabla haujafutwa na maelezo yake yote.

Pia kuna uzi niliandika kwa ajili ya mazoezi ya tumbo


Na wenyewe hauna maneno ila kuna watu waliniquote so utapata maelezo.

Kuondoa tumbo kunaanza na cardio kama vile kujog, kamba na aerobics. Kwa lengo la kuondoa tumbo nashauri baada ya muda uongeze juhudi katika mazoezi yako kwa kuongeza idadi na muda wa kufanya mazoezi.

Chakula unachokula siyo tatizo, tatizo lipo katika namna unayofanya mazoezi. Actually unatrain casually, so ongeza reps.
 
Kamanda eti pili pili ina madhara kwenye mazoezi?
Maana baadhi wanasema inakata pumzi!!!
Ndimu je?
Pilipili kwl inakata pumzi bro wang anacheza mpira akilaga msosi wa mchana hatumii kabisa pilipili na kama akitumiaga namuonaga uwanjan anavyokuw anahema kama mbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…