senzotakabora
New Member
- Jan 13, 2025
- 1
- 0
Fangasi miguuni (nyungunyungu) au athlete's foot kwa jina la kitaalamu, ni tatizo linalowasumbua baadhi ya watu.
Watu wenye tatizo hili mara nyingi hujikuta wakitumia tiba mbalimbali za kisasa bila mafanikio.
Kama mchango kwa jamii nimeona leo nishiriki na watakaojaliwa kupitia post hii, kuweka wazi tiba moja ya asili ambayo inaweza kuwasaidia wahusika kuondokana na tatizo hili kwa gharama ndogo kabisa.
TUMIA NJIA HII KUTIBU MAAMBUKIZI SUGU YA KUVU (FUNGUS) ZA MIGUUNI
Maambukizi ya kuvu ni tatizo linaloweza kumsumbua mtu kwa muda mrefu, na kumfanya atumie gharama kubwa sana kujitibu bila mafanikio.
Unapojikuta katika mazingira kama hayo tumia mchanganyiko ufuatao kujisaidia.
MAHITAJI
1. Majani ya muorobaini kiasi cha gram 500
2. Siki nyeupe (Acetic acid) kiasi cha lita mbili
3. Maji masafi kiasi cha lita tano.
4. Kitunguu saumu kibichi kiasi cha gramu 250.
MAANDALIZI
1. Chukua majani ya muarobani na vitunguu saumu na kuponda pamoja hadi kupata kinyunye laini.
2. Changanya kinyunye hicho na maji na kuchemsha kwa dakika kumi na tano (15), kisha uchuje na kupata kizuduo (extract)
3. Baada ya kizuduo kupoa changanya na siki na kuhifadhi kwenye chombo safi kikubwa cha kioo, udongo au plastiki.
MATUMIZI
Kila siku baada ya kuoga, kabla ya kulala usiku, chukua kiasi cha hicho kizuduo na uweke kwenye chombo mfano wa beseni, na kuroweka miguu hadi kwenye vifundo. Acha miguu ndani ya hicho kizuduo kwa dakika 10.
Tiba hii ina uwezo wa kutibu kabisa kuvu ndani ya siku 3.