Jinsi ya kutumia "Compound Interest" kwenye mafanikio

Seif Mselem

Senior Member
Joined
Oct 16, 2023
Posts
161
Reaction score
526
Kabla Albert Einstein Hajafariki mwaka 1955 Aliwahi kusema Moja ya Maajabu Nane ya Dunia (8th Wonders Of the World) ni "Compound Interest"

Najua litakuwa SIO Neno geni kwako ila tu labda hufahamu ni Jinsi gani unaweza kulitumia kupata Mafanikio ambalo hilo sio Kosa lako bali ni MFUMO wa Maisha yetu Kibongo.

Kwa sababu hiki kitu kinatumika sana kwenye Taasisi za "BENKI" kwahiyo Mtu inabidi akijue

Kwahiyo kwa leo nitakwambia Maana yake ki benki benki halafu baada ya hapo nitakwambia maana yake kwenye MAFANIKIO nitakupa na Mfano mmoja then tutamaliza kwa kuona Jinsi unavyoweza kuitumia kwenye kupata Mafanikio kwenye Kitu chochote kile unachofanya.

Hiyo Iko Sawa kwa Upande Wako?..

Yeah Vizuri!

Kwa maana ya Benki, Compound Interest ni Pesa uliyoweka kwenye Akaunti yako ya Benki na kisha unapata Faida (Interest) na Hiyo Faida (Pesa) inajiongeza kwenye Mtaji wako (Principal) kisha tena unapata Faida kwenye hicho Kiasi kipya kilicho Ongezeka na baada ya Muda pesa yako Inaongezeka kwa Kasi

Angalia mfano hapa...

Tuseme umeweka Tsh 100,000 kwenye Bank [ X ] halafu baada ya Mwezi Inaongezeka Inakuwa Tsh 110,000 kwahiyo sasa mwezi Unaofuata Mtaji wako hautokuwa tena

~Tsh 100,000~ Bali ni Tsh 110,000/= Kwahiyo baada ya Miaka labda 5 unajikuta na Pesa Nzuri

Umeona Jinsi inavyo Kwenda?..

Hiyo kwenye Ishu ya Benki na ishu zingine za Kifedha

Kwenye Mafanikio... Compound Interest Inatokana na kitu kimoja kinaitwa "Postive Feedback Loops (PFL). (Ondoa Shaka Nakwambia Maana Yake Hapa)!

PFL ina maana ya kwamba ni Mabadiliko madogo anayofanya Mtu ambayo baada ya muda yanaleta Compound Interest

Nimekuacha?..

Usijali! Cheki Mfano huu hapa chini [emoji1313]

...Kuna utafiti ukiwahi kufanya na wana Sayansi kuhusu samaki aina ya "Goldfish"

Kwamba ukiwachukua Samaki hawa wenye ukubwa na Kila kitu ambacho ni Sawa Halafu ukawaweka kwenye Bwawa (Pond) moja, Kisha ukamchukua mwingine Ambaye amewazidi wale kwa ukubwa na kila kitu japo kwa asilimia moja 1%, Yaani kama tunapima kwa miaka awe kawazidi mwaka mmoja tu

Utafiti unaonesha kwamba yule samaki aliyewazidi wenzake kidogo Ndio atakuwa kiongozi mule ndani ya Bwawa na yeye ndie atakuwa haraka kulinganisha na wengine wote kwa sababu atakuwa na uwezo wa kula chakula kingi kuliko wengine na kila kitu... Atawazidi!

Sasa hii ina maana gani kwenye Maisha yetu na Jinsi gani tunaweza kuitumia Kufanikiwa?

Yeah Vizuri!

Ukweli ni kwamba ukitaka kuwa Bora zaidi ya washindani wako basi Angalia ni kitu gani wote mko sawa halafu angalia kitu ambacho wengine hawana Ndicho ukifanyie kazi Ili ukiongeze kwenye kile unachofanya

Mfano Wewe ni Mcheza Mpira wa Miguu, Kitu ambacho wachezaji wengi hukosa ni "Winning Mentality"

Hata bongo hiki kitu kina Wasumbua wengi kwa sababu timu ikifungwa tu Hasa hasa dakika za Mwisho wachezaji wengi hukata tamaa

Kwahiyo Ili wewe uwe juu zaidi yao kwa Asilimia Moja inatakiwa ujifunze kuwa na hiki kitu Na hiki kitu Ndicho baada ya Muda kinapelekea kuwa wenda ukawa "Team Captain" n.k

Na hiki kitu kimojo ambacho kinaitwa "Positive Feedback Loop”. Ndicho kimewafanya wachezaji wakubwa kama Messi na Ronaldo kuwa pale

Kwa sababu kama wangefanya kama Wanachofanya wengine Basi hata Mimi na wewe tusinge wapenda kiasi Hicho

Kwahiyo kwenye sehemu yoyote ile ya Maisha, kama ni Biashara, Elimu, Mapenzi, Fashion, Sanaa, Chochote kile Angalia watu wengi Mna kitu gani cha Kufanana halafu wewe Ongeza ambacho wengine Hawana

Halafu baada ya Muda utanipigia Simu kunambia... Mselem Sipingani na Wewe

Hicho kitu ndicho kinachofanywa na Kila mtu aliyefanikiwa... Wanakuwa Atua Moja Mbele "One Step Ahead Of the Crowd"

By the way...

I Hope Umejifunza Kitu!

Uwe na Usiku Mwema

seif Mselem
 
Asante umeeleza vizuri sana

value preposition[B/]
 
Mimi ni Mchumi ila nimetoka na kitu mastaa, thank you man
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…