Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Udalali wa ardhi na majengo unahusisha huduma za kitaalamu zinazotolewa na madalali katika shughuli za kuuza, kununua, au kukodisha ardhi na majengo. Hapa kuna muhtasari wa masuala muhimu katika udalali wa ardhi na majengo:
Uuzaji wa Ardhi na Majengo.
Madalali wanasaidia wateja wao kuuza mali zao kwa kutangaza, kusimamia maonyesho, na kusaidia katika majadiliano ya bei.
Madalali wanahakikisha kuwa nyaraka zote muhimu zipo na kwamba mchakato wa kisheria unafuatwa ipasavyo.
Ununuzi wa Ardhi na Majengo.
Madalali wanawasaidia wanunuzi kutafuta mali inayofaa kulingana na mahitaji na bajeti zao.Madalali wanatoa ushauri kuhusu thamani ya soko na hufanya ukaguzi wa mali kabla ya ununuzi.
Ukodishaji wa Ardhi na Majengo.
Madalali wanasaidia katika kuunganisha wapangaji na wamiliki wa mali, wakiwasaidia kusaini mikataba ya ukodishaji.
Madalali wanasimamia mchakato wa ukodishaji, ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa kodi na utatuzi wa migogoro kati ya wapangaji na wamiliki.
Thamani ya Mali.
Madalali hutathmini thamani ya mali ili kuhakikisha bei inayopendekezwa ni sahihi na inaendana na soko la sasa.
Huduma za Ushauri.
Madalali wanatoa ushauri kuhusu masuala ya uwekezaji, maendeleo ya ardhi, na mikakati bora ya kuuza au kununua mali.
Mchakato wa Kisheria.
Madalali wanajua sheria na kanuni zinazohusiana na ardhi na majengo, na wanasaidia kuhakikisha kuwa shughuli zote zinafanywa kwa kufuata sheria.
Kwa ujumla, udalali wa ardhi na majengo unahitaji ujuzi wa soko, uelewa wa sheria, na ujuzi wa mawasiliano ili kusaidia wateja kufanikisha malengo yao katika soko la mali isiyohamishika.
Moja ya kazi nzuri za kujiingizia kipato kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo ni kutoa huduma za udalali wa ardhi na majengo.
Je unawezaje kuanza kutoa huduma za udalali wa ardhi na majengo mpaka kujenga mkondo wa kuingiza kiasi kikubwa cha kipato endelevu kila mwezi?.
Leo ninakushirikisha jinsi unavyoweza kuwa dalali wa ardhi na majengo mpaka kufikia mafanikio makubwa kupitia uwekezaji huu.
Mambo 5 Ya Kukumbuka.
Moja.
Jipe Muda Wa Kuanza Kuuza.
Jipe muda wa kuanza kuingiza kiasi cha kipato kutokana na huduma zako. Kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa huduma zako kinatakiwa kuwa ni cha matangazo zaidi.
Biashara ya huduma za udalali wa ardhi na majengo sio njia ya mkato ya kujenga mafanikio makubwa ndani muda mfupi. Utahitaji uvumilivu mkubwa huku ukiendelea kuwa mwenye bidii, uaminifu na kujifunza kwa bidii.
Ni huduma unayoweza kuandaa barabara ya kukutana na bahati ambazo zinaweza kubadili kabisa hali yako ya kiuchumi.
Hali yako mbaya ya kiuchumi inaweza kuboreshwa kwa kutoa huduma bora kwa uaminifu bila kuacha. Kwa maneno mengine sio biashara unayoweza kufanya miaka miwili au mitatu na kujenga mafanikio makubwa.
Usiwe na haraka ya kutaka mafanikio ya mwaka mmoja au miezi sita. Inawezekana ukapata mafanikio makubwa ndani ya miaka miwili kwa bahati tu.
Lakini kwa kawaida utatumia zaidi ya miaka miwili (2) kuanza kuchuma matunda ya biashara yako ya huduma za udalali wa ardhi na majengo.
Mbili.
Jenga Wafuasi Wako.
Ni muhimu mno kujenga mtandao wa watu wanaokufuatilia. Njia kuu za kuwapata wafuasi wako kwa haraka ni mitandao ya facebook na instagram.
Lakini hakikisha unatengeneza makundi ya WhatsApp na Telegramu kwa ajili ya kujenga mahusiano ya karibu sana na wafuasi wako.
Usisahau kutumia majukwaa makubwa yaliyo na watu wengi kama vile Jamiiforums na makundi mengine yanayohusiana na uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Mimi nimepata wasomaji wazuriwa huduma zangu kutoka kwenye jukwaa la Jamiiforums kupitia makala ninazoandika huko.
Tatu.
Kuwa Na Njia Kuu Ya Kuwafikia Watu.
Njia hii inatakiwa iwe ni njia isiyo ya moja kwa moja. Njia zisizo za moja kwa moja za kuwafikia wateja wako ni kama ifuatavyo;-
✓ Kutoa huduma za ushauri za udalali wa ardhi na majengo.
✓ Kutoa huduma zinazoendana na ardhi na majengo kama vile ujenzi, ukarabati wa nyumba, uandaaji wa ripoti za ukaguzi wa nyumba, elimu ya ukaguzi na ukarabati wa nyumba, upambaji wa nyumba, na kadhalika.
Kwa kuwafikia watu kupitia njia zisizo za moja kwa moja itakusaidia sana kuwa na kundi kubwa la watu ambao watabadilika kuwa wateja halisi au mabalozi wa wateja wako.
Nne.
Notibuku Ya Kumbukumbu Za Taarifa Zako.
Unatakiwa kuwa na notibuku nzuri na imara za kuanzia shilingi elfu tatu na kuendelea. Notibuku hii unatakiwa kuandika ripoti zifuatazo;-
✓ Namba za simu za watu wote ambao wanahitaji huduma zako pamoja na majina yao.
✓ Namba za simu za watu wote ambao wamewahi kuulizia huduma zako za udalali wa ardhi na majengo.
✓ Orodha ya ahadi zote ambazo wateja halisi na wateja watarajiwa wamekupa.
✓ Orodha ya majina ya wateja halisi na wateja watarajiwa pamoja na namba zao za simu.
Kutenga Asilimia Ya Kamisheni Unayopata.
Unatakiwa kutenga asilimia ya kipato unachotengeneza kila mwezi au mwaka. Zipo njia rahisi za kuanza kutengeneza fedha kwa mtaji mdogo sana kama vile kumiliki mabanda au makontena kwa ajili ya kupangisha.
Ni muhimu sana kuchagua njia unayoweza kuitumia kuwekeza kwenye ardhi na majengo. Usikubali kuwa dalali miaka mitano, kumi, au zaidi huku unaendelea kuwa huna kipato endelevu.
Kumiliki Nyumba Za Kupangisha.
Unaweza kununua nyumba ya kupangisha kwa mkopo wa mwenye nyumba (seller financing). Kwa njia hii unaweza kulipia nyumba ya kupangisha hata kwa kiasi kidogo cha fedha.
Na utaendelea kuipangisha kwa wapangaji huku ukiendelea kurejesha mkopo wa mwenye nyumba. Kwa kuwa wewe ni dalali itakuwa rahisi kupata mwenye nyumba aliyehamasika sana kuuza nyumba yake.
Tumia kazi yako ya mkononi udalali kununua viwanja na nyumba kutoka kwa wauzaji waliohamasika sana. Njia pekee muhimu ya kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba au kiwanja ni kununua kutoka wamiliki waliohamasika sana.
Hamasa huchochea mazingira mazuri sana ya mazungumzo yenye manufaa pande zote mbili. Kwa kufanya mazungumzo rafiki kati yenu mnaweza kupata njia ambayo inatatua changamoto zenu.
Kupata Uzoefu Kupitia Huduma Za Udalali.
Hakikisha biashara yako ya huduma za udalali wa viwanja na nyumba zinakusaidia kwenye kujifunza mambo yafuatayo;-
✓ Ramani za nyumba za zinazoingiza kiasi kikubwa cha kodi ya kila mwezi.
✓ Kukagua kitaalamu ardhi au majengo ya aina tofauti tofauti.
✓ Kuthamini ardhi na majengo.
✓ Kufanya tathmini za makisio ya jumla ya gharama za ujenzi.
✓ Kufahamu hali za soko mahalia na uchumi mahalia.
✓ Kuandika ripoti za ukaguzi wa nyumba au ukaguzi wa ardhi.
✓ Kufanya tathmini za mikopo ya majengo.
Ukiwa na maarifa sahihi kwenye maeneo haya itakusaidia kuongeza kiasi cha kipato endelevu chako. Utaweza kumiliki nyumba za kupangisha zenye kipato kizuri kwa bei nafuu.
Weka vipaumbele kwenye kujifunza vitu hivi niliyokushirikisha hapa huku ukiendelea kutoa huduma za udalali wa ardhi na majengo. Kumbuka kuwa ni kosa kujihusisha na udalali wa vitu vingine kwa sababu utakosa ubobezi hasa kama hauna kampuni.
Unahitaji kubobea kwenye udalali wa viwanja, mashamba na majengo ili kuvuta fursa zinazohusiana na ardhi na majengo. Ubobezi utakusaidia kujenga mtandao sahihi kuhusu ardhi na majengo.
Muhimu; Karibu unishirikishe chochote kuhusu somo hili. Una maoni, mapendekezo na ushauri karibu unishirikishe muda huu.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Calls/WhatsApp; 0752 413 711