Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,012
- 5,571
Maji ya Uwaridi na Liwa:
Liwa ina sifa ya kunyonya mafuta usoni na hivyo husaidia kutibu chunusi. Changanya Liwa na Maji ya Uwaridi kwa ratio ya 2:1. Paka usoni na uache hadi ikauke kabisa kisha osha na maji ya uvuguvugu. Fanya hivi kila siku na utaona mabadiliko baada ya wiki tatu za matumizi.
Maji ya Uwaridi na Multani mitti:
Changanya Multani na Maji ya Uwaridi hadi uwe uji mzito. Paka usoni na uache hadi ikauke kabisa kisha osha na maji ya uvuguvugu. Hii Multani ni udongo fulani unatumika sana India. Inapatikana kwenye maduka ya vipodozi.
Maji ya Uwaridi na Maji ya Limao:
Maji ya Limao yanaweza kumaliza kabisa tatizo lako la chunusi. Changanya Maji ya Limao na Maji ya Uwaridi kwa uwiano sawa, kisha paka kwenye ngozi ya uso iliyo safi na uache kwa dakika 10. Kisha osha uso vizuri.
Maji ya Uwaridi na Unga wa Dengu( Gram Flour):
Changanya Gram flour na Maji ya Uwaridi hadi uwe uji mzito. Paka usoni na uache hadi ikauke kabisa kisha osha na maji ya uvuguvugu.
Maji ya Uwaridi, Tango na Asali:
Kama una matatizo yanayosababisha usitumie Limao, hii itakufaa. Changanya tango, asali na maji ya uwaridi na upake usoni. Acha kwa muda wa dakika 15-20, kisha osha vizuri.
Disclaimer:
1. Usipake hivi vitu usoni kwa siku mbili au tatu ukategemea matokeo chanya. Consistency is the KEY. Matokeo huchukua hata mwezi kutokea ila huwa ni mazuri.
Ngozi hutengenezwa nje na ndani. Kuwa makini na unachokula, ndicho kinadetermine uzuri wa ngozi. Kuna wenye ngozi zao mashaallah hazihitaji effort, ila wengi wetu tunahitaji kutunza sana ngozi zetu ndipo tuzifurahie. Matunda na MbogaMboga viwe bestfriend wako. Tena ukila vibichi ndo unapata manufaa zaidi.