Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Itumie simu yako ya Android kama rimoti ya TV
Hivi unafahamu kuwa unaweza kuitumia simu yako ya Android kama rimoti (Remote Control) kwenye kifaa cha kielektoroniki chochote kile kitumiacho rimoti?
Kuna aina nyingi sana za TV, AC au DVR kwenye matumizi yetu ya kila siku ambayo hutumia rimoti. Mara nyingi imekuwa vigumu sana kupata rimoti nyingine ya kifaa chako pale kile cha awali kinapopotea au kuharibika.
Kutokana na uvumbuzi zaidi, sasa unaweza kuitumia simu yako ya Android kutatua janga hili pale linapokufika.
Unachotakiwa kufanya ni kupakua App ya IR Universal Remote + WIFI kutoka kwenye Google Play hadi katika simu yako na kisha itakupa maelekezo ya namna ya kuiseti na kifaa cha kilektrokini chochote kile kinachotumia rimoti na hivyo kutatua maswahibu yako.