Jinsi ya kutunza afya ya Figo

Jinsi ya kutunza afya ya Figo

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Figo hufanya kazi ya kuchuja damu kwa kuondoa maji na uchafu.

799891B3-75E6-480F-8F7D-2C1B41745592.jpeg


Aidha, hufanya kazi za kuweka uwiano sawa wa tindikali na alkali za damu, kutengeneza sukari kwenye nyakati ambazo mwili wa binadamu huwa na upungufu mkubwa wa sukari, kudhibiti shinikizo la damu pamoja na kuzalisha vichocheo vya calcitriol na erythropoietin ambavyo huusaidia mwili kufyonza vizuri madini ya calcium pamoja na kutengeneza damu.

Ili figo ziweze kufanya kazi hizi kikamilifu, unashauriwa kufanya mambo yafuatayo-
  • Kunywa maji ya kutosha kila siku. Kiwango cha lita 1.5-2 kinatosha kabisa kukuweka salama.
  • Usivute sigara, kemikali zake huathiri mishipa ya damu ambayo hupunguza mzunguko wa damu kuelekea kwenye viungo hivi. Kitendo hiki ni hatari kwa afya ya figo.
  • Epuka kutumia dawa pasipo kupata ushauri wa wataalamu wa afya. Aidha kumbuka kuwa siyo kila kitu cha “asili” ni salama. Tumia kwa uangalifu.
  • Tunza uzito wa mwili. Magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari na figo huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutokea kwa watu wenye uzito mkubwa.
  • Kama unaugua ugonjwa wa kisukari au shinikizo kubwa la damu unashauriwa kutumia dawa zako vizuri bila kuacha. Magonjwa hayo ndiyo chanzo kikubwa cha kufeli kwa figo.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara ili kutunza utimamu wa afya yako kwa ujumla.
Chanzo: NIDDK
 
Kwann figo sijui firigisi za kuku huwa zinakuwa na mawe mengi?

Au firigisi na figo ni vitu viwili tofauti,
 
Back
Top Bottom