Jinsi ya kuua biashara yako

Jinsi ya kuua biashara yako

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

JINSI YA KUUA BIASHARA YAKO

Inasemekana kwamba Biashara nane au tisa kati ya biashara mpya ambazo huwa zinaanzishwa huwa zinafeli, yaani zinakufa na zinashindwa kuendelea. Inaaminika kwamba asilimia hamsini (50%) ya biashara mpya zinazokufa huwa zinakufa ndani ya mwaka wa kwanza, asilimia zilizobaki huwa zinakufa ndani ya miaka mitano hadi tisa inayofuata. Ukichunguza unaweza kupata jibu, mana wengine Idea zinafia vichwani hata kabla hawajaanza utekelezaji.

Ukitaka kuua Biashara yako anza kuamini katika kupata faida katika kipindi cha muda mfupi. Watu wengi sikuhizi akitaka kuanza biashara atakuuliza, Man Dea nisaidie Idea ya biashara ambayo itanipa faida nyingi na kurudisha hela yangu ndani ya muda mfupi. Juzi kuna mtu aliniuliza hivi nikamjibu simple tu "Ushafeli". Chukulia mfano wa Azam TV na ile investment iliyowekwa pale, sitaki kuamini ndani ya miaka 2 atakua ameanza kutengeneza faida, ila naamini baada ya miaka 5 atakua anatengeneza super profit.

Amini watanunua na kukusapoti kwakua una Biashara. Watu wengi tukianzisha biashara cha kwanza ni kutafta rafiki zetu na kuwaambia na kuwaomba watuunge mkono kwa bidhaa zetu, well kwa hawa rafiki na familia wanaweza wakanunua na kukuunga kwa sabababu wanakujua, vipi kuhusu wateja wengine? Bidhaa zako zina ubora? Huduma zako ni nzuri na zina kiwango? Nikitaka huduma ya muda mrefu, kampuni yako ita exist mpaka kesho au itafia njiani tuanze daiana? Jiulize unaingiajje katika Soko, unaenda ukabili vipi Ushindani, Una kipi kipya au kizuri zaidi cha ku-offer wa wateja. Itaendelea.........
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA

By Man Dea
Instagram: Elimu_biashara
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom