Jinsi ya kuukaribisha umasikini

Jinsi ya kuukaribisha umasikini

Jini mtuu

Member
Joined
May 22, 2022
Posts
45
Reaction score
53
JINSI YA KUUKARIBISHA UMASKINI
1. ENDEKEZA USINGIZI
Kamwe usiamke mapema, endelea kulala na kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.

2. USIPANGILIE MATUMIZI
Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako, wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha kaa chini na jifikirie umezitumiaje.

3. USIWEKE AKIBA
Kamwe usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave vipi pesa zako wakati unazo kidogo? Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema katika matumizi yako.

4. USIFANYE BIASHARA ZA KIMASKINI
Kamwe usijiingize katika biashara ambazo huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na kiyoyozi.

5. SUBIRI MTAJI MKUBWA
usifikiri kuanzisha biashara mpaka pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni kukuletea mtaji wa kuanzia biashara. Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama kina Bakhresa walianza kuuza mgahawa, wewe ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika biashara zako.

6. ENDELEA KULALAMIKA
Lalamika kuhusu kila kitu, isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na attitude yako. Ilaumu serikali, zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha, zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya hawataki kukufanya uwe tajiri!

7. MATUMIZI YAKO YAZIDI MAPATO
Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata. Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki nunua gari kali, watoto wa mjini wakukome.

8. USIPITWE NA FASHENI
Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua Samsung Galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita halaf ongezea hela ukanunue Sammsung Galaxy S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu bhana.

9. NUNUA GARI MBOVU
Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari ya mtumba ambayo gharama zake za kulihudumia ni mara mbili ya mshahara unaoupata, au gari linalokaa muda mrefu gereji kuliko barabarani.

10. WADEKEZE WANAO
Wape wanao kila wanachokitaka kwa kuwa wewe ni mzazi bora, hawatakiwi kuhangaika wala kufundishwa utu na thamani ya pesa, usiwafundishe juu ya kutunza na kuheshimu fedha. Usiwafuatilie kabisa katika masomo yao.
Waache wakue wakiwa wavivu na waje kuwa masikini kuhakikisha kuwa hawawezi kukusaidia pale utakapozeeka.

12. KULA BATA
Tembelea viwanja vyote vya bata, na uzuri wamiliki wa maeneo ya starehe wanatujali yaani wanafungua maeneo mapya kila siku, tembelea yote. Kula bata kula bata.

13. Ongezea lililosahaulika....

Na ukishakuhakikisha kwamba unatekeleza hayo yote, kaa chini na utafakari kuwa siku zote fainali nzuri huchezwa uzeeni!
 
Namba 4 hapo nakazia kila mwanachuo anataka awe muuza simu tena iphone ,au nguo Tena udalali wanaacha fursa zenye pesa nyingi ili wabaki kuzurura hapa dar kusifia tu hii iphone used toka Dubai mara hivi uchawa tu kweny maduka pale kariakoo na makumbusho kupiga picha

Wote wamekuwa wauza nguo na mikoba
 
kuuepuka umaskini ni kuacha kujichanganya na maskini.

maskini hao ni:
maskini wa akili na mawazo.
maskini wa sio jua kubadilisha tabia zao na mbinu ya kijikwamua.

leo kajipendekeze kwa mtoto wa bhakharesa kama utakuw maskini basi umerogwa
 
Namba 4 hapo nakazia kila mwanachuo anataka awe muuza simu tena iphone ,au nguo Tena udalali wanaacha fursa zenye pesa nyingi ili wabaki kuzurura hapa dar kusifia tu hii iphone used toka Dubai mara hivi uchawa tu kweny maduka pale kariakoo na makumbusho kupiga picha

Wote wamekuwa wauza nguo na mikoba
Fursa zenye pesa nyingi ni zipi mkuu...

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom