JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kabla ya kugusa barakoa, safisha mikono yako na Sanitizer au maji na sabuni.
Kagua barakoa kuona kama imechanika au kama ina matobo, usitumie barakoa ambayo imewahi kuvaliwa au imeharibika.
Kisha, tambua ndani ya barakoa ni wapi, kwa kawaida ndani huwa upande mweupe.
Weka barakoa yako usoni ukifunike pua, mdomo na kidevu, hakikisha kwamba hakuna nafasi zilizowazi.
Weka kamba nyuma ya kichwa chako au masikio.
Usipishanishe kamba kwa sababu hii inaweza kusababisha uwazi kwenye baadhi ya sehemu.
Kumbuka, usiguse sehemu ya mbele ya barakoa ukiwa umeivaa ili kuepuka maambukizi; ukigusa kwa bahati mbaya, safisha mikono yako.