Jinsi ya kuwachuja wagombea Ubunge maelfu waliotia nia kupitia CCM

Jinsi ya kuwachuja wagombea Ubunge maelfu waliotia nia kupitia CCM

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Mimi nimeshiriki interview nyingi na najua maswali ya mitego watia nia wakiwa wengi hata wajae uwanja wa taifa wakigombea nafasi moja.

Kuisaidia CCM kuchuja hao maelfu walioomba ni kazi ndogo tu na rahisi

Swali moja tu la kwanza la kuwachujia ni kuuliza matawi waliko wanapoishi wameyasaidiaje matawi hayo ya CCM kihali na mali ? Pili kwenye hayo majimbo wanayogombea wamesaidiaje Ofisi za CCM kwa hali na mali?

Wengi wameibuka tu. Wanaijua CCM kwenye kugombea tu kutafuta mishahara mikubwa na miposho ya bunge lakini kabla ya kugombea hawakuwa na mpango na CCM iwe kwenye matawi yao wanapoishi au majimbo yao. Wengine hata jina la mjumbe wao wa nyumba kumi hawamjui
 
We nawe hewa kbs, tupo uchumi wa viwanda...tunataka wagombea WASOMI, hatutaki tena Kibajaji type!

Watia nia walete chamani CV zilizoshiba, ndio maana hata baraza la mawaziri linalomaliza muda wake mh Rais alipata wakati mgumu sn kutafuta watu wenye uwezo hadi mtu kama Kangi Lugola naye eti ktk nchi ya watu zaidi ya ml 50 anakuwa Waziri!
 
We nawe hewa kbs, tupo uchumi wa viwanda...tunataka wagombea WASOMI, hatutaki tena Kibajaji type!

Watia nia walete chamani CV zilizoshiba, ndio maana hata baraza la mawaziri linalomaliza muda wake mh rais alipata wakati mgumu sn kutafuta watu wenye uwezo hadi mtu kama Kangi Lugola naye eti ktk nchi ya watu zaidi ya ml 50 anakuwa Waziri!!.
Kibajaji,Musukuma&Goodkuck Mlinga ni watu wa muhimu sana kwny Chama Chetu.

Wale ni special kwa ajili ya kutoa matusi kwa upande wa pili.
 
Aina ya mchujo huko ni simu tu inapigwa kutoka kwa mwenye chama. Huyu mukate yure mupitishe so hakuna haja ya kuumiza kichwa
Mfano:Mwenye Chama alishatangaza, "Kuna Wengine Wanaenda Kuchukua Fomu Kule Geita Wamtoe Musukuma Kure"

Kabla Hujagombea Jiurize Umefanya Nini Zaidi Yake
 
Wanaccm wajanja wamewekeza majina Yao Kwenye tuezi mbalimbali huko mbele ya Safari haya mazingaombwe unayoyaona ni mitego imetegwa mara baada ya kuisha uchaguzi watateuliwa Tu na mwenye chama...

Wewe lofa mtoa mada utaishia Kwenye levo ya buku7 tu
 
Majina ya kupita anayo mwenyekiti, hizo mbinu zako baki nazo. Hakuna mtu ana muda wa kwenda kusaidia sijui tawi au nini, wakati hizo ofisi ni za kupigia Majungu, ushirikina na kila uchafu unaoujua ww. Hiyo ccm sio taasisi ya kihivyo, bali mbwembwe zote ziko kwenye madaraka ya rais.
 
Mkuu Yehodaya, mbona maswali yako yalishatolewa majibu na Mwenyekiti Taifa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM hivi juzi kati tu. Kumbuka jibu kwa yule kada kutoka Songwe na hatimaye mabadiliko madogo ya katiba yaliyofanyika ili kuweza kuwafanya wanachama wapya kupata sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi sawa kabisa na wale wa zamani.
 
Back
Top Bottom