Jinsi ya kuwapata wabunge na majimbo ya uchaguzi kwa washirika wa muungano

Jinsi ya kuwapata wabunge na majimbo ya uchaguzi kwa washirika wa muungano

Mshombsy

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
372
Reaction score
180
Kuna sababu tano zinazofanya nchi zinazoendelea kuongeza maeneo ya kiutawala kama mikoa au wilaya. Kwanza ni kisingizio cha kusogeza huduma karibu na wananchi kitu ambacho si kweli mfano tumeongeza mikoa mingi tokea uhuru lakini taifa halina hospitali inayojitosheleza kivifaa mfano mlipuko wa mabomu Olasiti Arusha, kumbuka mkoa wa Manyara umemegwa toka Arusha lakini hakukuwa na hospitali ya kuweza kutibu baadhi ya majeruhi, pili ni gerrymandering yani kuchezea mipaka ya majimbo ya uchaguzi ili kutoa nafasi kwa chama au kundi fulani. Tatu ni kisingizio cha kuondoa migogoro ya kikabila, nne ni Serikali kuu kuwa na uwezo mdogo wa kukataa shinikizo la wananchi wanaotaka mkoa au wilaya yao. Tano ni kulipa fadhila za kisiasa kwa kuteua wakuu wa mikoa au wilaya mpya na kutengeneza ajira mfano mganga mkuu wa mkoa hii yote kwa wanamtandao waliofanikisha mtawala kuingia madarakani.

Sababu zote hizi zinaweza kudhibitiwa ikiwa kuna utaratibu unaoeleweka juu ya kuongeza maeneo ya kiutawala kwenye katiba mpya. Kama sababu hizo zikitumiwa na mshirika mmoja wa muungano basi hazitohathiri mshirika mwingine wa muungano. Rasimu ya katiba inatamka ibara 105(3) kwamba kila mkoa kwa Tanzania Bara na wilaya kwa Zanzibar itakuwa majimbo ya uchaguzi. Rasimu haitamuki mwenye mamlaka ya kuongeza mikoa upande wa bara au wilaya upande wa zanzibar hivyo kuacha mwanya kwa washirika wa muungano kutumia sababu nilizotaja kujiongezea idadi ya wabunge.

Mtizamo wangu katiba mpya itamke idadi kamili ya wabunge wa muungano wakuchaguliwa kwanza na wagawanywe kulingana na idadi ya watu toka kila upande wa muungano. Hivyo lazima katiba itamke uwepo wa sensa itakayosimamiwa na chombo kimoja kila baada ya miaka 15 (mfano) ikifanyika miezi 18 kabla ya uchaguzi mkuu. Katiba pia itamke mwenye mamlaka ya kushughulikia mipaka ya majimbo ya uchaguzi.

Chombo chenye mamlaka ya kushughulikia mipaka ya majimbo kitapewa takwimu za sensa katika makundi mawili kama ntakavyoyaelezea na kuzichambua kupata idadi ya watu wa kujumuishwa kwenye ugawaji wa wabunge kwa pande zote za muungano. Chombo hiki kikimaliza hesabu zake kitawajulisha washirika wa muungano idadi ya wabunge kila upande itayopata kulingana na idadi ya watu wake miezi 12 kabla ya uchaguzi mkuu. Washirika watatenga majimbo ya uchaguzi kulingana na wabunge waliopata.

Makundi mawili ya watu watakaojumuishwa kwenye takwimu za sensa kuwapata wabunge: Kundi la kwanza ni watu wote wanaoruhusiwa kupiga kura. Kundi la pili ni wasioruhusiwa kupiga kura ikiwemo walio chini ya miaka 18, wageni wenye ukazi wa kudumu, wageni wenye biashara au ajira za mikataba ya muda mrefu. Kundi hili la pili litajumuishwa kwa kutumia moja ya sita yani kila watu sita itahesabika moja na kuongezwa kwenye kundi la kwanza. Mfano kama kundi hili la pili litakuwa na watu laki 6, basi laki 6 itagawanywa kwa 6 na kupata laki 1 itakayoongezwa kwenye kundi la kwanza kupata idadi kamili. Kundi la pili kanuni yake ina lengo la kutoa usawa kwa walipa kodi hao hata kama sio raia kwani watapata huduma nyingine hata kama hawapigi kura, na watoto chini ya miaka 18 kuna mtu ambaye anabeba jukumu la kuwatunza na ndiye huyo anatakiwa kufanya maamuzi bora kuchagua viongozi. Baada ya sensa na kufanya hesabu Tanzania Bara itakuwa na idadi B ya watu na Zanzibar itakuwa na idadi Z. Ukijumlisha B na Z utapata idadi J ya watu wa Jamhuri ya Muungano.

Inawezekana kukatokea upande mmoja wa muungano ukawa na idadi ya watu zaidi ya asilimia 99 ya watu wote ndani ya muungano hivyo kufanya upande mwingine usiweze kupata mbunge hata mmoja. Ili litaondelewa kwa katiba kutamka kwamba kila upande wa muungano utakuwa na uhakika wa wabunge V. Hivyo kabla ya kugawa wabunge baada ya sensa wabunge 2V watatolewa na kubaki wabunge M watakaogawanywa kwa washirika.

Mfano katiba ikisema kutakuwa na wabunge X=120 wa bunge la muungano na V=10 basi M=X-2V=100 na ndo wabunge watakaogawanywa kwa washirika kwa mtindo wa wingi wa watu. Baada ya sensa ikatokea B= 1,750,000 na Z=750,000 basi J=B+Z=2,500,000. Mgao wa wabunge itakuwa kama ifuatavyo: zidisha M na idadi ya watu (B au Z) ya mshirika kisha gawanya kwa J (idadi ya muungano) na jibu itakuwa mgao wa mshirika uliyetumia.

Hivyo Zanzibar yenye watu Z itapata wabunge 30 na ukiongeza V=10 kila mshirika anaohakikishiwa basi itawakilishwa na wabunge 40 wa kuchaguliwa. Ni jukumu la zanzibar kutenga majimbo 40 ya uchaguzi na majimbo lazima yawe na idadi RZ ya watu sawa au inayokaribiana, hivyo kila jimbo Zanzibar litakuwa na watu RZ=18,750. Tanzania Bara itawakilishwa na wabunge 80 na itatenga majimbo 80 na kila jimbo Bara litakuwa na watu RB=21,875.

Ili kuongezwe majimbo (wabunge) baadae katiba itamke kanuni juu ya idadi ya watu ambayo ikiongezeka baada ya sensa wabunge wataongezeka. Mfano kama idadi iliyoongezeka JT inakaribia mara 10 ya wastani wa idadi ya watu ya jimbo moja Zanzibar RZ na jimbo moja Bara RB, basi majimbo yatakayoongezwa ni namba kamili bila kukadiria baada ya kugawanya JT kwa jumla ya RZ na RB. Mfano kama JT ni watu 198,527 basi itagawanywa kwa jumla ya 18,750 na 21,875, jibu lake ni 4.8868 ila kwasababu tunachukua na kamili wabunge wataongezeka wanne.

Kanuni hii ina sharti linalotokana na rasimu ya katiba ibara ya 28(1) inayosema kila mtu ana haki ya kuishi popote atakapo ndani ya Muungano. Kama ongezeko JT linaonekana upande mmoja wa mshirika huku upande mwingine idadi yake ikipungua hakutakuwa na ongezeko la wabunge. Hii inaweza kuwa watu wameamia upande mmoja wa muungano kutafuta maisha. Hii itafanya majimbo kubadilika kila baada ya miaka 15 baada ya sensa. Mfano wetu hapo juu ikiwa JT ingeonekana yote imetoka Zanzibar na imepungua toka Tanzania Bara, idadi mpya ya watu kwa washirika: B = 1,750,000 - 198,527 = 1,551,473 kwa bara na Z ni 198,527 + 750,000= 948,527 kwa Zanzibar. Idadi ya watu wa muungano J=2,500,000 haitabadilika kwasababu watu waliamia Zanzibar. Ukipiga mahesabu Zanzibar itaongeza wabunge saba na kufikia 47 toka 40 na Tanzania Bara kupoteza wabunge saba mpaka 73 toka 80. Hii itabadili idadi ya watu kwenye majimbo ya uchaguzi mfano kila jimbo Zanzibar litaongezeka watu kufikia 20,181 wakati bara watupungua mpaka 21,253.

Hitimisho: mfumo wa kugawana wabunge kwa wingi wa watu katika shirikisho hautoi usawa kwa washirika, unaweza kushindwa kuondoa manung'uniko hivyo nchi nyingi ziliamua kuweka mabunge mawili (Bicameral). Bunge la juu (seneti) lenye wawakilishi wachache wenye busara na weredi kwa idadi sawa toka pande zote za muungano, chini ya makamu wa rais na mwenye kura ya uhamuzi ikiwa kura ni sawa. Hii yote ni ili ikitokea mswada umepita seneti basi kuna upande umeungana na mwingine kuupitisha na si upande mmoja. Bunge la pili ni la chini linalopatikana kwa wingi wa watu kama nilivyolielezea. Lengo ikiwa muswada umepita bunge moja, jingine liuangalie kwa jicho la pili.
 
Ninadhani suluhisho la uchumi katika nchi hii,ni viongozi kupigia chapuo serikali za majimbo,sababu mapato yote yanayopatikana yatabaki ktk jimbo husika, na hii itawapa changamoto majimbo mengine kuhakikisha wanatoza kodi,
 
Hii naona ndiyo maaana ajira inakuwa shida sana kwa sisi vijana endapo mki penetret hiyo kuhusu representative tanzania itarudi enzi za nyerere .
Viongozi wa tanzania na maanisha CCM iko siku itawatokea puwani.tumwombeni mungu atufikishe mwaka 2015 mungu atajuwa ndiyo dereva wetu
 
Hii naona ndiyo maaana ajira inakuwa shida sana kwa sisi vijana endapo mki penetret hiyo kuhusu representative tanzania itarudi enzi za nyerere .
Viongozi wa tanzania na maanisha CCM iko siku itawatokea puwani.tumwombeni mungu atufikishe mwaka 2015 mungu atajuwa ndiyo dereva wetu

Mi ni kijana pia ila sidhani kama umeisoma na kuielewa. Irudie tena vizuri. Kuwepo na utaratibu kikatiba sio kila rais anaongeza wilaya, mikoa na majimbo. Katiba mpya kenya imetamka idadi kamili, nigeria, na marekani waanzilishi wa hii kitu.
 
Back
Top Bottom