Jinsi ya Serikali kuondoa lawama na kutuhumiana kuwa wawekezaji toka nje wanatuibia

Jinsi ya Serikali kuondoa lawama na kutuhumiana kuwa wawekezaji toka nje wanatuibia

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Mara nyingi kumekuwa na msemo kuwa wawekezaji wa nje wezi wanatuibia waafrika .Hatufaidiki na uwepo wao au tunafaidika kidogo wao ndio wanapata Sana kwenye mikataba ya madini,mafuta ,gesi nk

Tatizo kwenye hili ufumbuzi tunao sisi wenyewe waafrika.Nitatoa mfano makampuni yanayochimba mafuta,madini,gesi nk yamesajiliwa kwenye masoko ya hisa ya kimataifa ambako Mtu yeyote aweza kwenda kununua hisa kule hata mtanzania wa kawaida angeweza nunua hisa za Baricck nje ya nchi kwenye soko la hisa .

Sasa Kama raia watanzania tungekuwa tunaruhusiwa na serikali zetu za kiafrika kununua hisa za haya makampuni makubwa ya hisa kule nchini kwao yanakotoka Ina maana sisi wenyewe waafrika faida wanayopata kule nchini kwao mgao tungepata Tena kwa hela za kigeni.Na tungetembea kifua mbele kama wamiliki wa Barick

Kwa hiyo kampuni ikija Africa hata ibebe makinikia ili ikapate faida kubwa kwao sisi hiyo faida ingetuhusu sababu Ni wamiliki wa kampuni hiyo kule kule kwao

Serikali za kiafrika ziruhusu waafrika raia wa nchi zao ikiwemo Tanzania kununua hisa masoko ya hisa ya nje ya nchi ndipo tutazalisha matajiri wengi.Kampuni zote kubwa za uwekezaji zilizopo nchi zetu za kiafrika ikiwemo Tanzania kule Ziko masoko ya hisa ya kimataifa .Tutarget income at the source tuache tu kutuhumiana ohh huyu mwekezaji mwizi mwizi.

Serikali za kiafrika ikiwemo Tanzania ruhusuni ,raia wenu waanze kumiliki haya makampuni ya kigeni ya uwekezaji yaliyoko nchi zenu na hata yaliyoko nchi zingine Duniani kwa kuruhusu raia wenu wakanunue hisa kule kwao kwenye masoko yao ya hisa.

ukiwa na hisa tena kwao hakuna wa kukudhulumu ni haki bin haki
 
mada yangu imekosa wachangiaji kulikoni?
 
Back
Top Bottom