Habari wote jamani, ni kweli inabidi mods watusaidie kuhusu kuziunganisha hizi maana mamabo mengi tunajifunza hapa, kila mara ninarydi hapa na kuchota mambo mapya.
Sasa kuhusu chakula naomba nikushauri kwa kuanzia jaribu kununua hata starter tu kwa wauzaji wazuri, kichunguze sana uone harufu rangi na texture yake, waweza kusaga kiasi kwa ajili ya finisher huku ukiangalia kuku wanakuwaje. mfano mashudu mengi bila mahindi kwenye finisher yanafanya kuku wako anakuwa mafuta mengi sana ila uzito hana na mahindi mengi paraza yanasaidia uzito mkubwa kwa kuku, vilevile uongezaji wa kuku bora inasaidia ukingaji wa magonjwa mbalimbali,
Nakushauri nunua mifuko michache ya kuanzia, nunua vitu vyote vinavyohitajika kwa kusaga kwenye mashine mfano 'Hill...' iko maeneo ya Bunju njia ya bagamoyo wanasaga na kuuza hivyo vyakula na vikorokoro vyoote vinavyohitajika. Unakuwa na chakula chako kama backup na cha kununua hadi ujue jinsi gani kuku wanakula, wanaadhiriwa na vyakula. Round ya pili utakuwa umeishajua ufanye nini moja kwa moja. Kama unatoka mbali waweza nunua vitu muhimu tu na mahindi na vitu vingine ukaenda nunua jirani na shamba lako. Naweka mchanganuo niliwahi pewa na mfugaji mwenzangu unasaidia, pia na mwongozo kidogo wa ufugaji toka wizara husika. Usisite kuwauliza mashine kama formula yako imepunguka vitu wanaweza kuwa msaada zaidi.