Jinsi ya upimaji wa engine oil katika gari lako

INJECTION TECHNICIAN

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2020
Posts
356
Reaction score
794
NI vyema kupima oil ya GARI lako kabla ya kuanza safari.

Na muda mzuri wa kupima oil nI pale gari lako linapokuwa limepaki kwa muda kufikia oil yote kushuka na kupoa hasa asubuhi unapoamka kwa sababu oil na engine vyote vinakuwa vimepoa kabisa.

Saizi salama ya Oil ya gari lako unapoipima ni kwamba oil yako haifikii alama ya MAX kwenye geji na haishii kwenye alama ya MIN yaani kwa maneno rahisi isifike kwenye max na isikomee kwenye alama ya min

images (6).jpeg
 
NI vyema kupima oil ya GARI lako kabla ya kuanza safari
Na muda mzuri wa kupima oil nI pale gari lako linapokuwa limepaki kwa muda kufikia oil yote kushuka na kupoa hasa asubuhi unapoamka kwa sababu oil na engine vyote vinakuwa vimepoa kabisa.
Saizi salama ya Oil ya gari lako unapoipima ni kwamba oil yako haifikii alama ya MAX kwenye geji na haishii kwenye alama ya MIN yaani kwa maneno rahisi isifike kwenye max na isikomee kwenye alama ya min
Ikizidi max inaweza kupelekea shida gani?
 
Nitajuaje ubora wa oil iliyopo kwenye injini kama bado ipo kwenye ubora au la?
Ubora wa oil hutegemeaana
.1; aina ya oil uliyotia
2;umbali ulotembelea chombo chako tangu utie oil(hamuwezi kuwa sawa katika ubadilishaji oil kati ya usafiri binafsi na usafiri wa umma kwa maana ya kwamba usafiri wa umma huzunguka kilometer nyingi kwa siku chache tofauti na chombo binafsi ambacho hutumika kwendea kazini kikisubiri jioni kurudi nyumbani)

Uborara wa oil unaweza kuangalia kwa kuchunguza viscosity kwa lugha nyepesi ule mnato wa oil unapoishika na hata rangi yake itakuonesha imetumika kiasi gani Kama ipo ndani ya engine ikiwa ya kahawia bado unaweza kutumia kiasi Ila ikiwa nyeusi NI dhahir unatakiwa ubadilishe
 
Shukran mkuu. Kipengele hiki ulisahau kuweka ndio maana nikauliza, kwasababu najua ukaguzi wa vimiminika kwenye gari hauishii kwenye kuangalia ujazo tu.
 
Naomba utujuze kuhusu wajerumani
BMW wamekua na tabia ya kutoweka dipstick kwenye magari. Kwahiyo asubuhi unawasha gari, unasubiri kama dk 5-10 hafu unapima level kwenye computer iliopo ndani.
IMG_0599.jpeg

Hii kitu inakera asubuhi ukiwa na haraka asubuhi basi tu.

Mi nilikua nacheki oil level muda wa kurudi kazini au nikitoka home nitakapo simama au kwneye jam ndio nacheki.

Maana inahitaji gari likae on kama dk -15 hivi.
 
Back
Top Bottom