Top Gun
Member
- Dec 11, 2024
- 49
- 171
Miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni ilikuwa ni golden age ya filamu za nollywood haswa zile za kichawi. At last, vitumbwi vya maisha ya Kiafrika vilikuwa televised kupelekea watu kuguswa na matukio yale na kuyaunganisha/kurelate katika maisha yao.
Miaka hio ndio baba ameanza kushika pesa, nyumba kali huku kukiwa na special shelf ya mikanda ya filamu za aina nyingi. Filamu zile tulizitazama sana na kati ya zile kuna filamu ambazo zilikuwa zikionesha baba anaoa mke wa pili then mke wa pili analeta ushindani wa kishirikina. Kutokana na udogo wetu tulijua hii ni entertainment tu lakini we were deeply wrong, masikini, hatukujua kama ipo siku mimi na ndugu zangu tutakuwa sehemu ya filamu ya kinaigeria.
Picha linaanza baba kukutana na mrembo mmoja huko alipokuwa ameenda kikazi katika wilaya ambayo sio mbali na makao yetu (1 hour drive). Single mother mmoja hivi wa watoto wawili (kila mtoto baba yake) ila ulikuwa ukimuona unaweza kudhania hajawaahi kwenda labour. Alikuwa na kila kitu ambacho mwanaume yoyote yule angetamani kuwa nae. Alikuwa anashighulisha na kutembeza mitumba ya watoto na wanawake.
Wakati huo ndio ulikuwa core ya ugomvi wa baba na mama. Baba na mama walikuwa wameshaanza kuzinguana, mara mama anaondoka baba anamfata. Na kiasili baba alikuwa mkali na mbabe sana. Mama pia alikuwa ni mtu wa kuzila sana, kwa hio mzee aliona dawa ya mama ilikuwa ni ngumi. Na ilikuwa mama akisepa anaondoka na wadogo zetu wadogo zaidi kuhofia kutopata malezi bora kutokana na udogo wao.
Lakini cha kushangaza ilikuwa mama akisepa baba anayumba sana kimaendeleo, kusema kweli mzee alipata mama mchapakazi, hongereni wasukuma. Kusepa kwa mama kuliwapa mwanya wifi yake (shangazi yetu ambae pia alikuwa anamchomea sana mama) kujipigia mapesa katika biashara za mzee maana palikosa usimamizi mkuu maana baba na yeye alikuwa ana shughuli nyingine.
Tulikuwa watoto wanne, sisi wawili wa kiume ndio tulifatana (2 year difference), hawa wengine (mapacha wa kike) walizaliwa tukiwa tumewapisha miaka kama saba kutokana na matatizo ya uzazi ya mama pia na ile vurugu za baba na mama kutokukaa tulii. I am the second born na first ndio alikuwa the most handsome (warembo walikubali sana in his teens), mshapu, charming (ucharming ulilemletea shida moja hivi mbeleni), mkorofi, friendly na pia very creative.
After some time, Tulianza kupata za chini chini kutoka kwa mama kuwa baba yenu ana mwanamke mwingine na amempangishia na huyo mwanamke amezaa nae mtoto mmoja ila ana watoto wengine ambao hana uhakika kama ni wababa maana mmoja ana asili kama ya kiarabu hivi (half cast) na mwingine na hakufanania na baba kabisa.
Siku moja wakati nipo likizo, baba alikuja nyumbani na gari, "ebu panda chapu hapa nikupeleke sehemu moja hivi unisaidie kurekebisha kitu fulani"
Ndani ya ile gari kulikuwa na milango mipya ya mbao na fremu zake. Sasa kutoka na ukauzu wa baba niliogopa kumuuliza ni ya wapi hio milango. Tulienda hadi ile wilaya B na tukashuka mtaa mmoja ambao katika wilaya umepewa jina la utani la uswahilini.
Tulipofika tukamkuta bibi mmoja amekaa pembeni (akiwa mwenye uzuni) na vijana wawili wakiwa na vifaa vya kiufundi. Tulivyofika tukaisaidiana kushusha milango ile hadi kwenye hio nyumba alipokuwa amekaa bibi huyoo (ni nyumba hizi matope za zamani ila imepigwa lipu kifundi maiko).
"Kijana msalimie bibi yako huyu"
mimi: "shikamoo bibi"
bibi: "huyu ni mwanao? , duuh amefanana kama yule wa xxxx, kweli damu yako ni kali sana"
mzee akaacheka na akasema taratibu atawajua tu ndugu zake wengine.
Duh moyo wangu ulishtuka na nikajua direct huyu atakuwa mama yake huyo mwanamke aliezaa na baba.
So tulikuta pale milango imevunjwa kama vile amevamiwa. Niliomba kwenda msalani kukujoa, mmoja ya watoto wa wadogo pale akanionesha, nikaingia. Nilivyoingia , kama unavyojua hivi vichoo vya uswailini juu hamna paa kwa hio sauti za nje unaisikia kirahisi sana.
Mara nikasikia watu wanapita kando na nikasikia sauti ya kike ikisema "mmh yani huyu bibi kila siku anavamiwa yeye tu, sasa ana kipi cha kuibiwa, huyu itakuwa, amevaruga watu flani na mauchawi yake , sasa wanataa kumzuru"
Yule mdada mwingine akasema "yani ashukuru anaishi na kijana wake mdogo, (wakiume), atamlinda"
Duuh muda ule moyo ulishtuka ila mara hii hadi tumbo lilivuruga hadi nikaamua kufanya longa call badala ya shortcall 😂😂.
Nini kinaendelea baada ya hapo, tukutane kesho wakuu.