Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Maalim Seif akizungumza na Mwandishi (haonekani kwenye picha) nyumbani kwake Dar es Salaam
Mwandishi akimkabidhi Maalim Seif kitabu cha Kumbukumbu za Ali Muhsin Barwani ''Conflict and Harmony in Zanzibar.''
Kumtembelea Maalim Seif nyumbani kwake ni mfano Waingereza wangesema ‘’a walk in the park,’’ Kiswahili chake labda mtu ungesema unatoka chumbani kw.ako unakuja sebuleni yaani ni wepesi usiomithilika. Maalim nimefahamiananae kwa mara ya kwanza 1992 nilionananae Starlight Hotel Titi Street, Dar es Salaam. Hizi zilikuwa siku za mwanzo za siasa za vyama vingi.
Miaka mingi imepita na hapa katikati tukionana kwa mbali sana na kwa muda mfupi mfupi ile ya kupeana salaam, Waswahili wanausemi, ‘’salaam ya Mungu,’’ ikiwa na maana mnasalimiana kisha mnapitana kila mtu na hamsini zake. Lakini namini Maalim akinisoma na wakati mwingine akinisikia katika vyombo vya habari, pia wakati mwingine akipata salaam zangu kupitia jamaa na marafiki. Lakini mimi Maalim nimenfuatilia kwa karibu na nimempiga picha nyingi sana kwa kiasi ya miaka ishirini na zaidi.
Leo nimepata bahati ya kumfikia nyumbani kwake Sharif Shamba nje na mbali na matarumbeta na shamrashamra za mikutano na mengineyo. Ilikuwa starehe tukinywa kahawa na kucheka mfano tuko barzani tunapumzika. Lakini tabu kukutana na mtu kama Maalim Seif ukaacha kumdodosa lau kwa mbali kwa namna ya maskhara. Najua kitabu cha Ali Muhsin kakisoma kilipochapwa tu mwaka wa 1997 lakini niliona nimepelekee kuchokoza upya fikra zake.
Mimi binafsi katik kitabu cha Ali Muhsin moja ya sehemu iliyokamata fikra zangu ni pale anapohadithia yale aliyokutananayo katika jela mbalimbali za Tanganyika wakati alipofungwa baada ya mapinduzi. Nikamrushia Maalim swali, ''Maalim tupate basi kitabu makhsusi ulipokuwa kifungoni.'' Kacheka kidogo. Nilikuwa nimemkumbusha mbali. Jibu lake lilikuwa, ''In Shaallah.'' Sikumuacha karibu nikaongeza na ''Memoirs...'' yaani kumbukumbu za maisha yake. Mara ya mwisho kuwa jirani sana na Maalim ilikuwa mwaka wa 2012 Bwawani Hotel nikiwa na TV Imaan tulikokwenda kumsikiliza Maalim akizungumza kuhusu hali ya Zanzibar na mategemeo ya wananchi.
Maalim alikuwa sasa yuko serikalini. Nakumbuka shida niliyowapa walinzi pale nilipoingia katika chuma cha faragha alipokuwa Maalim Seif, Mzee Hassan Nasoro Moyo na viongozi wengine. Mimi nilikuwa nje na wala sikuwa na nia ya kuingia ndani ya chumba kile kwani mtangazaji na mtu wa kamera tayari walikuwa ndani ya chuma kile wakishughulika. hawa vijana wote wana vitambulisho shingoni vinaning'inia na watu wa usalama weshawaruhusu.
Mimi sina chochote lakini Ismail Jussa ndiye kanishika mkono tunazunguma basi hadi mle chumbani nikawa sasa uso kwa uso na Maalim. Ikawa sasa tunazungumza hili na lile, ''easy.'' Sasa nimefungua ''tablet,'' yangu nampiga picha Maalim na wakati mwingine kumwelekeza ''pose,'' niitakayo. Kumbe jamaa wa Usalama kidogo weshafanya wasiwasi wa kutaka kunijua mie nani. Mara niko kwa Mzee Moyo tunazunguza na kucheka. Lakini jamaa wa Usalama bado hawajanijua mie nani. Mara nimerukia Eddy Riyami basi ikawa kwao wao ni tafrani kidogo. Nilipotoka nje tu wakanifikia kwa maswali...
Mwandishi akiwa Viwanja Vya Jangwani akifuatilia mkutano wa CUF na kupiga picha mwaka wa 2000
Jicho halisahau kile ambacho jicho la kamera liliona. Naomba kamera yangu ikuchukue katika barabara ya kumbukumbu turudi nyuma zaidi ya miaka ishirini iliyopita pale nilipoanza kufuatilia nyayo za Maalim na wale aliokuwa pamoja na yeye...
Fatilia ukurasa huu...In Shaallah tunautengeneza....
View attachment 381663
Historia mpya ya Zanzibar bila shaka watakapokuja kuandika watafiti wa historia ya visiwa hivi itatoa umuhimu wa pekee katika uchaguzi wa mwaka 1995. Kwa mara ya kwanza wananchi wa Zanzibar walitikisa na pengine mtu unaweza kusema walivunja ngome ya dhana ya, ''Mapinduzi Daima.'' CCM Zanzibar walishindwa uchaguzi ule. Imewezekana vipi kwa kipindi cha miaka mitatu tu ya uhai wa CUF ikaweza kuwa na nguvu ya kupambana kukishinda katika sanduku la kura chama kilicho na dola na fursa zote zinazokwenda na dola. Tume ya Uchaguzi Zanzibar ilishindwa kutoa matokeo ya uchaguzi kwa siku tatu. Yaliyobakia ni historia.
Endapo Maalim ataandika kumbukumbu zake sura hii ya uchaguzi wa mwaka wa 1995 utakuwa na mengi ya kusisimua. Mwandishi alikuwapo Zanzibar kipindi kile na aliiona hali ya Zanzibar kwa jicho lake. Kitu ambacho anakikumbuka ni siku baada ya matokeo kucheleweshwa akiwa amekaa Malindi akamuona Baraka Shamte katika magwanda ya kijani akipita barabarani huku akipiga makelele mathalan ya mtu aliyepagwawa akisema, ''We have won the election we are going to form the government.'' Lakini kitu cha ajabu hata wale CCM waliokuwa wamezagaa katika vikundi vidogo vidogo walikuwa kama wamenyeshewa na mvua. Walikuwa kimya wakizungumza kwa sauti za chini. Taarifa zilikuwa zimewafikia kuwa Maalim Seif Sharif Hamad kashinda uchaguzi na kamwangusha Komando Salmin Amour.
View attachment 381665
Kalenda ya Maalim Seif kuingia Ikulu Zanzibar 1995 ilikuwa imewekwa kwenye maskani maarufu CUF ''Jaws,'' Stone Town
Mwaka wa 2012 baada ya miaka 17 kupita na hali ya siasa za Zanzibar kubadilika, Maalim na CUF wakipata nguvu kila kukicha nilifanya mahojiano ya televisheni na Baraka Shamte, kada mkubwa wa CCM na mwana ASP. Wakati huu Maalim alikuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar. Nimepata kumjadili Baraka Shamte mara kadhaa katika mitandao ya kijamii. baraka Shamte ni mtu mwenye histroia kubwa katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964. Baraka Shamte ametunukiwa nishani ya miaka 50 ya mapinduzi.
Mwandishi Akifanya Mahojiano na Baraka Shamte Kada Maarufu wa CCM Nyumbani Kwake Mkunazini Zanzibar Kuhusu Historia ya
Mapinduzi. Baraka Shamte ni Mtoto wa Mohamed Shamte Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Zanzibar Aliyepinduliwa Katika Mapinduzi ya 1964
Uchaguzi wa Mkuu Zanzibar 1995 Mwandishi akiwa nje ya kituo cha kupiga kura Darajani siku ili mvua kubwa ilipiga.
Shaaban Mloo na Walid Kabourou kampeni za uchaguzi wa 2000
Nilipokutana na Maalim kwa mara ya kwanza aliniuliza uwezekano wa CUF kupata wanachama Bara.
Kushoto: Prof. Ibrahim Lipumba, Shekue, Mama Ummie na Ummie biti yake