Jioni moja na Maalim Seif Sharrif Hamad

Mkuu sipendi uiite hadithi! Hii ni Historia ya kusisimua sana! Asante
Capt...
Uniwie radhi ndugu yangu lakini wakati mwingine huwa
tunachukua lugha ya barza ili tusiwaudhi wengine.

Mara kadhaa nadhani ushanisikia hapa majlis khasa jamaa
wanaponiangushia makombora baada ya kuwapa ya ndani
ambayo wao hawakuyategemea, mie husema, ''Hakuna neno
si lazima uniamini...''

Hakika ni historia ya kusisimua.

Iko siku CUF walitaka signature 200 zipatikane katika saa 8
ili ziwahi ofisi ya Msajili asubuhi saa 4 siku ya pili.

Taarifa wametuletea usiku baada ya sala ya Isha.

Jua halijapanda siku ya pili asubuhi signature 200 ziko mezani
kwa Maalim akague.

Alichoka.

Hawa walikuwa wakifanya kazi hii kiatu chao kanda mbili.
Hawaulizi posho wala nauli ya safari.

Wanakula rakaa moja kwa siku.
Watu dhalili kwa hali lakini wana mioyo mikubwa.
 
Historia adhimu, mzee said tunaomba uandike tanzia ya maalim seif in shaa allah kama itakupendeza.
 

Sasa wale wanaotwambia kuwa chama kilikua cha mapalala wao wanasimama na hoja ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…