Jipatie Mtaji - kwa wazo zuri la biashara

Jipatie Mtaji - kwa wazo zuri la biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Watu wengi tumekuwa tukilalamika kuhusu kukosa mitaji ya kufanya biashara na kutuwezesha kujiajiri. Ukosefu wa mitaji umekuwa ni kilio cha vijana, wazee, walemavu, wakina mama na kila mtu. Hata mimi ni mmoja wa hao ambao nilifikiri kwamba nahitaji mtaji ili niweze kutimiza malengo yangu.

Katika kufanya biashara na ujasiriamali mdogo kuna mambo mengi ambayo nimekuwa nikijifunza hasa pale biashara yangu inapoanguka na kujikuta nikipata hasara.Binafsi nimewahi anzisha biashara tofauti nyingi sana na kujikuta nikipata hasara hata pale ninapokuwa na mtaji mkubwa. Nimefanya biashara ndogo,za kati na hata zile kubwa za mitaji mkubwa,nimefanya biashara za uchuuzi, huduma, na hata kuwekeza katika kilimo na maeneo mengine. Lengo langu lilikuwa ni kuweza kufanikiwa.kimaisha.

Katika tafakari yangu ya maisha yangu ya biashara na hasa kushindwa kwangu katika biashara niligundua kwamba tatizo langu kubwa halikuwa kwenye kupata mtaji bali lilikuwa ni kwenye kupata wazo bora la biashara"Ingelikuwa Rahisi kupata mawazo bora na mapya ya Biashara,hakuna mtu angeajiriwa "Kila siku watu wangekuwa wanaazisha biashara mpaya a kuwa mabilionea."

Tafakari yangu imenifikisha katika hatua ya kutambua kwamba wengi wetu tunafikiri kwamba tatizo ni mitaji lakini ukweli ni kwamba tatizo ni kwamba hatuna Business Idea ambayo inalipa. Hatuna Bankable projects ideas. Ni ukweli kwamba hata hilo wazo lako ulilo nalo linaweza kuwa sio bankable idea,

Sio kila idea unayookoteza barabarani na kwenye mitandao na kwenye vijiwe ni idea ambayo inaweza kuwa biashara.Idea nyingine ni kama filamu tu kwa ajili ya kusisimua imaginmations zako na kuchangamsha ubongo ila hazifai kufanyiwa kazi na wala haziwezi kudumu kama biashara.Huu ni ukweli mchungu kwa wale ambao tunahamasisha watu wajiajirii,wawe wajasiriamali lakini ni ukweli ambao lazima useme kwamba TATIZO SIO MITAJI,TATIZO WATU HAWANA IDEAS ZA BIASHARA ZINAZOELEWEKA.Wengi wanaokoteza tu ideas hapa na pale Basi kisha wanasema wanataka mitaji.

  1. Mambo muhimu katika uzalishaji wa kibiashara ni pamoja na(Factors of Production)Land,Labor,Capital,Entrepreneur.Wazo lolote la kibiashara ni lazima litimize vigezo ambavyo ni muhimu sana ili kuhakikisha kwamba linafanikiwa.
    1. Moja ya vigezo hivo ni uwepo wa soko la uhakika?(Enough Demand to warant production)
    2. Uwepo wa Uwezo wa kuzalisha(Enough Supply capability to meet demand)
    3. Kuwepo na ugumu katika entry(Barrier to entry)Isiwe rahisi kwa mtu mwingine kuingilia biashara hio),
    4. Uwepo wa competitive advantage(Ushindani),
    5. Kuwepo na uwezo wa Kulisimamia na kuendesha(Management)
Mambo haya yote ni lazima yatazamwe kabla ya kudai kwamba unahitaji mtaji.Ukweli ni kwamba kama wazso lako halina vigezo hivo hata ukipewa mtaji hautafanikiwa.Ukweli ni kwamba wengi wanaosema hawana mitaji wanasema kama kisingizio cha kuficha ukweli kwamba hawana mawazo mazuri,au hawana uwezo wa kutekeleza mawazo yao au hawana uwezo wa kufanya biashara na kuwa wajasiriamali.

Ukitaka kuelewa ukweli jaribu kufuatilia historia za watu waliofanikiwa utagundua kwamba wengi wao kufanikiwa kwao hakukuja kwa bahati na wala hawakuwa na mitaji mikubwa bali walikuwa na mawazo ambayo ni solid na wakayanyia kazi kwa kadiri ya uwezo wao kwa wakti huo na kisha baada ya wazo kuanza kupata shape wawekezaji walijitokeza na mawazo yale yakawa jinsi tunavyoyaona sasa.

Ili nisiwaache watu wakiwa wamekatia tamaa mawazo yao kutokana na andiko hili naomba kidogo niseme kuhusu namna ya kutambua iwapo wazo lako linakidhi vigezo vya kuitwa wazo.Pamoja na maelezo mengine hapo juu ni muhimu wazo lako likalenga kutatua changamoto katika jamii inayokuzunguka au hata katika dunia. Kutegemea ni kiwango chako cha elimu na uzoefu, kuna mambo ambayo unaweza kufanya yakawezesha watu kuishi kwa furaha, katika mazingira bora, hayo ndio mambo ambayo unatakiwa utafuta namna ya kuyafanya yawe kibiashara.

Ukitazama mfano wa mitandao ya kijamii ambayo ililenga zaidi kuwawezesha watu kuwasiliana na sasa imekuwa sehemu ya biashara kutan gaza biashara zao,serikali kufanya tafiti za kijamii na matumizi mengine mengi ambayo usingewezakuyafikiri.Ukitazama mtandao ka JF ambao sasa umekuwa sehemu ya kupashana habara na kupeana elimu na zaidi umetoa ajira kwa watu wengi sehemu tofauti.Yote haya yalikuwa ni mawazo ambayo yalileta suluhisho fulani na yakaweza kupata shape na kuwa business idea.

Kwa hio unapofikiria kuhusu business idea usifikiri kuhusu profit margin,capital etc,fikiri kuhusu namna unaweza kutatua changamoto za kijamii,na kwa kupitia hapo unaweza kufikia malengo yako ya kibiashara kwa kuleta suluhu ambayo ina make business sense.

Kila la heri
 
It's a nice message somehow tho I don't agree 100%... Kuna aina nyingi za businesses.. Small and big Ones.. Hata level ya execution na demand ya mtaji vinatofautiana

Mi mwnyw nko na idea hapa.. Imekidhi vigezo vyako hivyoo.. Lakini am still struggling kupata mtaji.. But there's no turning back.. I'LL GET IT maana hata ROI yake ni nzuri kwa mtu atakayeinvest (500k per month)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,Surely Kama imekidhi vigezo vyote haiwezi kukosa mtaji,Mara nyingi ideas zote huwa hazitimizi vigezo vyote na hapo ndo concept ya risk taking inapoingia.Yaani kama idea in vigezo vyote inamaana risk yako ni ndogo sana ambayo inamaanisha kwamba mtu huwezi kuwa na hofu ya kuwekeza hapo kwani garantii ya faida ni kubwa.Ukiona idea inakosa buy in ujue ama inakosa kigezo fulani,au unaaproach wrong people,au hujaweza kuiuza.Ila idea ambazo hazina risk huwa zinaonekana kuwa ni too risky.Tushirikishane PM kisha tupeane ushauri zaidi.Karibu
 
Back
Top Bottom