Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Hii yawezekana ndio sababu CCM hawataki wananchi wengine wakipate?

 
Kwa kuweka kitabu hiki hapa, sijui mmewakosesha wahusika mapato kwa kiasi gani. Na sijui swala la copyright linakuwaje. Pale Great thinkers infringe copyright.
 
Kwa kuweka kitabu hiki hapa, sijui mmewakosesha wahusika mapato kwa kiasi gani. Na sijui swala la copyright linakuwaje. Pale Great thinkers infringe copyright.

not really.. hii haikuwa kwa ajili ya faida.... ni public domain..
 
not really.. hii haikuwa kwa ajili ya faida.... ni public domain..

Tutafuatilia kuona wangapi wamekisoma kupitia mtandao wa JF then tutazidisha mara kumi na tutafanya harambee ya kusadia Foundation ya Mwl. Nyerere.
 
Nilikuwa nimeamua kuchukua likizo na JF lakini imenibidi nikatize likizo yangu kwa sababu ya hii thread. Asante sana Mkuu SubiriJibu umenikumbusha mbali na hapa natokwa machozi nikitafakari hatma ya nchi yangu niipendayo Tanzania inavyonajisiwa hivi sasa na viongozi limbukeni. Mungu atusaidie, amina.
 

Mbona unataka kukimbia Mag3, ukiwa kama mdau unaweza kubadilisha hii forum pia kwa kuleta sred za maana kama hizi
 

- Wakipewa nafasi na sisi wananchi, ambao kama unayosema ni kweli basi ni malimbukeni kuliko hata hao viongozi, kwa sababu wanachanguliwa na sisi wananchi, au? Likizo imeisha mkuu? karibu sana tumkome nyani!

FMEs!
 
- Wakipewa nafasi na sisi wananchi, ambao kama unayosema ni kweli basi ni malimbukeni kuliko hata hao viongozi, kwa sababu wanachanguliwa na sisi wananchi, au? Likizo imeisha mkuu? karibu sana tumkome nyani!

FMEs!

Viongozi hawa hawapewi nafasi na wananchi, wanahakikisha wanajipa hizo nafasi kwa kutumia njia zozote zile. Ndio maana Mwalimu kwa wakati fulani aliwaita wahuni hawa kwani hata pale wananchi watakapowakataa, watatafuta jinsi ya kujihalilishia nafasi zao. Wapo watakaofanya juu chini kujaribu kufuta historia hata ikibidi kukana kauli zao wenyewe au kung'ang'ania uongozi hadi kufa. Ndio mkuu FMes, likizo imeisha na sasa Mag3 nimerudi tumkone nyani kisawasawa bila kumtazama uso, a luta continua.
 
when it comes to suala la mwl.JKN.......wengi hukurupuka pasipo hata ku-read btn the lines.....!At least baada ya kusoma mawazo yake kwenye kitabu chake hiki nadhani mawazo ya wengi humu ndani towards him yatabadilika! HEY GREAT THINKERS......WHAT DO YOU THINK OF THE MAN....?
 

Safi sana, hiki ni cha kuprinti na kusoma vizuri, Mungu amweke Mwl mahali pema peponi, nadhani haki miliki haitaleta shida.
 
Mwalimu anaendelea kusema katika UWHT..


Na kuendelea kugongomelea msumari:

Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga, si dalili ya heshima; na woga na heshima ni vitu viwili mbali mbali. Maadili mema hayatudai tuwaogope viongozi wetu.

na kutupa elimu hapa:

Hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa.

Na kama nabii pweke jangwani akasema:


Na kama Musa mbele ya wana Waisraeli walioasi nyikani akasema:

 

Tafadhali naomba uki"scan" na kukiweka kwenye mtandao. Ni muhimu kwa wadau kukipata
 
JKN yeye passion yake ilikuwa Muungano.alikuwa hataki kabisa serikali 3!Mnakumba group 55!Nimecheck hiyo attachment juu juu sidhani inazungumzia tatizo la sasa:Ufisadi!!!Ufisadi.

Tukumbuke JKN ndio alimtaka Mkapa !Angalia family ya Mkapa ilivyofanya:Kufanya biashara ukiwa ikulu na dubious Kiwira deals.

Hatima ya nchi hii sio JKN tena,hata tukisoma kitabu mara mia!Tukumbuke JKN aliua upinzani,kurecover imekuwa shida sana.Assume tungekuwa na akina Slaa tangu uhuru?Upinzani sio vita,ni kuimarisha demokrasia na kukosoana.SISIEM inavyobehave ni kama chama kimoja.Kila mtu anajua kukifund hiki chama fedha inatoka wapi.

I salute wale ambao walitaka kuleta mabadiliko ya kisiasa toka mwanzo.Chief Fundikira,Makwaia,Kasanga Tumbo,James Mapalala na wengineo wengi.
 
Mwalimu anaendelea kusema katika UWHT..



Na kuendelea kugongomelea msumari:



na kutupa elimu hapa:



Na kama nabii pweke jangwani akasema:



Na kama Musa mbele ya wana Waisraeli walioasi nyikani akasema:

Nukuu hizo zimetoa Muhtasari wa ujumbe uliokusidiwa. Hata kama sitasoma chote hapa ndiyo alimaliza kazi. Ndiyo maana kimefichwa na wahusika.
 
Nadhani sasa kiko kwenye posti ya kwanza..
MM Ulianza kupiga type ili uweze kutuletea hiyo nakala hapa? kwa kweli mzee kama umefanya hivyo nikupongeze huu ni moyo wa pekee kuhakikisha watu wanaijua kweli labda siku moja hiyo kweli itawaweka Huru. Ubarikiwe sana mkuu
 
MM Ulianza kupiga type ili uweze kutuletea hiyo nakala hapa? kwa kweli mzee kama umefanya hivyo nikupongeze huu ni moyo wa pekee kuhakikisha watu wanaijua kweli labda siku moja hiyo kweli itawaweka Huru. Ubarikiwe sana mkuu

hapana sikufanya mimi hii kazi. NI kutokana na chanzo cha kuaminika. Shukrani apewe "invisible". Ninachofanya sasa ni kukiweka sawa maana kina makosa mengi ya uchapaji, ni kama first or second draft..

Nyerere hakukawaia kuwaita wapumbavu viongozi uchwara..

 
Kwanza nikiri kuwa ni mmoja wa watu waliomisi hii kitu ila nashukuru kwa kuwekwa hapa hiyo hazina. Aisee huyu mzee aliipenda hii nchi hawa waliopo sasa wanapenda maslahi yao kwa kupitia nchi hii WHAT IS HE WAS ALIVE TODAY?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…