Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere


- Nimekisoma sana mkuu tena kwa kufundishwa na mama mmoja m-Jew aliyepona pona kwenye mauaji ya Hitler, historia haiandikwi na watawala that is my point.

Respect.


FMEs!
 

- Bob vipi ndugu yangu umerudi maana nimekutwangia sana, maneno mazito sana haya.

Respect.


FMEs!
 
Nipo, nipo Boingo mkuu wangu nachukua Phd ya Udalali! maanake nimeisha pigwa changa la macho natafuta nauli hivi! bwaaa bwaa bwaaa!
 

- Mkuu umeshawahi kujiuliza kwa nini hawa wabunge wa G55 hawakushikwa na uhaini, maana that is exactly walichokuwa wanakifanya, na kwa nini Kaseka kiongozi wa hili kundi alipewa uwaziri baada ya hizi vurugu?

Respect.


FMEs!
 
- Nimekisoma sana mkuu tena kwa kufundishwa na mama mmoja m-Jew aliyepona pona kwenye mauaji ya Hitler, historia haiandikwi na watawala that is my point.

Respect.

FMEs!

Mkuu kama historia haiandikwi na watawala inaandikwa na nani? Wanahistoria wanasema historia huandikwa na washindi. Ndio maana historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa imeandikwa na Wajerumani na Waingereza. Mpaka leo kitabu kikuu cha historia hapa nchini kinaitwa A MODERN HISTORY OF TANGANYIKA na kimeandikwa na Muingereza kwa jina John Iliffe.
 

- Ikiandikwa na watawala ndio matokeo yanakuwa kama hiki kitabu.

FMEs!
 
FMES halafu kumbuka Hitler hakuwa mtawala wakati anakiandika na tena hicho kitabu kwa kiasi kikubwa ndicho kilichomuuza wa Wajerumani mpaka wakamkubali - hebu soma rejea hii:

Hitler began the dictation of the book while imprisoned for what he considered to be "political crimes" after [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Beer_Hall_Putsch"]his failed revolution in Munich[/ame] in November 1923. Though Hitler received many visitors earlier on, he soon devoted himself entirely to the book. As he continued, Hitler realized that it would have to be a two-volume work, with the first volume scheduled for release in early 1925. The prison governor of Landsberg noted at the time that "he [Hitler] hopes the book will run into many editions, thus enabling him to fulfill his financial obligations and to defray the expenses incurred at the time of his trial."

Source: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Mein_Kampf[/ame]
 
Companero,
Alichofanya Nyerere kinaweza kutafsirika vyovyote vile.. Sidhani kama ni busara kwako wewe kuandika historia ya maisha yako mwenyewe..kwa mfano ktk historia hiyo kama uliachana na mkeo mara nyingi mbaya atakuwa mkeo kumbe kulingana na watu wengine wanavyoiiona picha wanajua fika mkorofi ni wewe.
Kifupi historia ya nchi yetu inajiandika yenyewe hadi leo hii nachokiona ni MIMBA tu...
 
Historia lazima ihifadhiwe kwa maneno au maandishi. Tatizo letu ni kuwa historia yetu hatuihifadhi ipasavyo. Ndio maana tupo hapa tunagombania Kitabu cha Nyerere kama pipi. Hizi ni historia ambazo zinapaswa kuwa wazi kwa kila Mwananchi. Tunapaswa kuwa na kumbukumbu ya kitaifa kuhusu haya masuala. La sivyo mafisadi wa jana leo tutawaita wapiganaji! Afadhali sasa tunaanza kuamka, Azimio la Arusha nalo linachapishwa upya kwa Kiingereza na Kiswahili. Tukikumbuka tulipotoka hatuwezi kuacha huu upuuzi wa sasa uendelee! Tuhifadhi kumbukumbu za nchi hii, tumetoka mbali!
 
FMES,

..unless kuna kitu ambacho sikifahamu, lakini kwa uelewa wangu Wabunge wale walikuwa wanatumia haki yao ya kikatiba ndani ya Bunge la Jamhuri.

..kuhusu Njelu Kasaka kupewa Unaibu Waziri labda ilikuwa ni njia ya kumnyamazisha. wengine kama Sebastian Rukiza Kinyondo[r.i.p] alipewa wadhifa wa ukuu wa mkoa.

..nimeelekeza kwamba hawa G-55 walikuwa wamekerwa zaidi ya rushwa iliyokuwa inafanywa na Mwinyi na kundi lake. kwenye hoja yao walikuwa mpaka na malalamiko kwamba wa-Zenj wanateuliwa kushika nafasi zisizo za muungano. kuwapa G-55 madaraka ilikuwa ni njia ya kuwaingiza ktk kundi la wenye ulaji.

NB:

..binafsi ningependa sana kusoma hoja ya Tanganyika kama ilivyowasilishwa na Njelu Kasaka, na zaidi kupata hansard na kumbukumbu za mjadala huo bungeni.
 
Jamani, PM Malecela alikuwa nacheza strategy nzuri sana ya "" no blood in my hands"" na kwa kweli angeshinda kama sio Mwalimu kuona mchezo mzima.

Huwezi kushindwa kuitetea Serikali bungeni ukabaki PM, no way.
Huwezi kwenda kinyume na CCM, halafu bado ubaki kiongozi wa serikali ya CCM.

So JKN was right.

Mabavu ya kumleta Mkapa hiyo ni topic nyingine, na vile vile kutuletea Mwinyi wakati alikuwa hana uwezo hiyo nayo ni topic nyingine.
 

Lakini si ilitosha kumwambia kwa uzuri mzee wa watu Mtei kuliko kumwambia anahisia za Ki-BBC?
 
Lakini si ilitosha kumwambia kwa uzuri mzee wa watu Mtei kuliko kumwambia anahisia za Ki-BBC?

Kweli mkuu. Ni jazba tu maana kila kona nakutana na hizi hisia. Sasa huwa inaniuma napokutana nazo kwa wazee wetu ambao wanapaswa kutuonesha njia vijana tunaopumbazwa na vyombo vya habari. Nahisi hii iliniuma zaidi maana ndio kwanza nimetoka kukisoma kitabu cha Mzee wetu. Samahani kwa kuumiza hisia zenu.
 
FMES, ..unless kuna kitu ambacho sikifahamu, lakini kwa uelewa wangu Wabunge wale walikuwa wanatumia haki yao ya kikatiba ndani ya Bunge la Jamhuri.

Ndugu yangu nadhani unasahau kuwa Katiba ya wakati ule bado ilikuwa na 'schedule' ya 'party supremacy', yaani Katiba ya CCM ilikuwa imeingizwa ndani ya Katiba ya Nchi hivyo kwa kiasi kikubwa Chama kilikuwa juu ya Dola na Mihimili yake ndio maana Mwalimu Nyerere aliwawakia hao Wabunge waliokuwa wanapingana na Sera na Ilani ya Chama chao!

Nashauri kitabu cha Tanzania! Tanzania! cha Mwalimu nacho kiwekwe humu maana kinaelezea hoja hiyo ya Chama kushika hatamu dhidi ya G55. Kuna sehemu kinasema hivi:

"Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hadhi ya bunge...Mimi nasema kuwa ["Wabunge"] wanayo haki hiyo ["ya kuhoji Katiba, ambayo si maoni bali ndiyo sheria kuu ya nchi yetu"] na uhalali huo. Lakini wanajivua haki hiyo kwa kutumia hoja za kijinga. Ati Bunge likishatamka maoni yake, hata kama maoni hayo hayana uzito wa sheria, vyama vyote, pamoja na chama kinachotawala, lazima viyaheshimu maoni hayo au sheria hiyo, na vifute sera zao, hata kama uamuzi wa Bunge au Wabunge ni kinyume na sera zao. Na hata kama Wabunge hawakutumwa na wapiga kura kupitisha sheria hiyo. Hivi ninyi mnafikiri udikteta unaanzaje?"

Nadhani wanasheria wanaweza kulieleza hili suala la nguvu ya kikatiba ya chama kimoja vizuri. Ukipata muda pitia makala hii ya mwanasheria mahiri: http://www.kituochakatiba.co.ug/Maina99.htm. Au soma vitabu vya Msekwa maana alisifia sana kitendo cha kuipa nguvu ya kikatiba dhana ya chama kimoja kushika hatamu kuwa ni kitendo cha aina yake katika historia ya utungaji/uundaji Katiba duniani!
 
mkuu, nimekisoma kwa haraka sana,
lakini mbona kina Typo nyingi sana? ndo chenyewe au draft?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…