Jipe moyo

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
WEWE NI NANI?



Kama mti uzaapo matunda basi ndio na sisi tunavyozaliwa.



Kuna matunda ambayo huotea chini na kuwa rahisi kuchumwa, haya hu represent wale watu waliobarikiwa kuzaliwa na visimati, na hawatumii nguvu nyingi ili kutimiza malengo yao.



Kuna yale ambayo huanguliwa hata kama yapo mbali, basi hawa ni watu wenye potential sana pamoja na kujiweka nyuma, au kukulia kwenye maisha magumu ila bado hubahatika kutoboa katika maisha.



Kuna yale matunda ambayo huchumwa yakiwa bado mabichi na kuvundikwa, basi hawa ni wale watu ambao tokea wadogo watu huwapigia mahesabu makubwa sana kutokana na tabia au talent zao.



Kuna yale matunda ambayo huanguka na kuoza chini, uchukuliwa na kufanywa kama mbolea ili kusaidia mazao mengine kukua.

Haya matunda yan represent watu ambao hutumika kukuza wengine, mfano umeoa mwanamke ambaye ni mama wa nyumbani.

Usimdharau kwasababu bila yeye huenda usingekuwa na amani, utulivu wa akili na ndio maana unafanikiwa, kwahiyo riziki zake hupita kwako.



Kuna yale ambayo unakuta yameliwa mtini na wanyama wengine, yamedonolewa. Haya matunda hu represent wale watu ambao wapo emotionally taken advantage of kutokana na wema wao, uzuri wao, in short kwasababu walikua vulnerable. Hawa huja kuwa motivational speakers wazuri, walimu wazuri na ndio ambao hutetea sana haki za watoto, wanawake, binadamu nk kutokana na experience walizopitia.



Kuna yale ambayo huozea mtini, haya hurepresent wale watu ambao unakuta alizingua kwa namna flani katika maisha kwahiyo huipa dunia nuru ya kujifunza kutokana na makosa, pia hawa watu ndio ambao husaidia watu wajifunze kutoka kwao na kutokurudia makosa.

Mostly haya matunda huanguka chini na mbegu yake ikiota basi husaidia mmea mwengine kuzaliwa, ndio kwamba hulipia makosa yao, na mwishowe hubadilika na kuwa mtu bora zaidi , stronger, mwenye maono makubwa katika jamii.



Point ni kwamba, hii itakusaidia kuelewa kuwa tunatofautiana, sio kwamba kila aliyefanikiwa sana basi ana akili mno kushinda wengine, au anajituma sana.

Hivyo usiumie , usiwe mwepesi wa kudharau au kuhukumu.

Kila mtu ana kundi lake katika dunia hii.



Nawatakia siku njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…