jipu kwa kiingereza linaitwaje?

Kwa kizungu rahisi ni BOIL. Umenikumbusha miaka yangu ya mwanzoni nilipoingia ulaya, nilipataga bonge la jipu- mwanzoni nililipuuzia mara likapasuka na usaha wenyewe ulikuwa na rangi kama ya hazurungi- sasa mgogoro ulikuwa ni namna ya kumulezea DR -JIPU, USAHA, HAZURUNGI.....ilikuwa kazi kwelikweli.
 
ABSCESS ndo jibu sahihi. Tumor ni result ya uncoordinated cell growth mf cancer!
 

Hahaha ulitamani uende mwananyamala hospital, pole mkuu nadhani ulaya ilikuwa inatoa vumbi vumbi na mabaki ya jasho ya Dar.
 
Boil si ni MCHEMSHO kaka...au hiki ni kiinglishi cha heshima ya bar....

Hapana,hajakosea mkuu,jipu kwa kiingereza rahisi ni Boil....'Boil:-A painful infected swelling under the skin which is full of the thick yellow liquid called Pus (Pus=Usaha)
 
Hapana,hajakosea mkuu,jipu kwa kiingereza rahisi ni Boil....'Boil:-A painful infected swelling under the skin which is full of the thick yellow liquid called Pus (Pus=Usaha)

Taib, sheikh!
 
Hapo ndipo ninapo aminia wanaJF mnamajibu yaliyoenda kidato hongereni sana
 
Mi sitii mguu hapa ni mweupeee kabisa sijui lolote kuhusu jina la jipu kidhungu!!!
 
jipu - 'abscess' au 'boil'. Kwa Kiingereza ya kila siku hamna utofauti kubwa kati ya 'abscess' au 'boil'. Ikitokea ndani ya mwili kwa kawaida hapo Uingereza tunasema 'abscess', kama ikitokea 'on the skin' kwa kawaida tunasema 'boil'.
"
Abscesses may occur in different parts of the body. Abscesses in the skin are know as boils." Haina maana sana kuhojiana kama ni 'abscess' au 'boil'. Inakaribia ziwe ile ile kwa lugha ya kila siku ya watu. Tumour ni tofauti kabisa na abscess/boil.
abscess / boil - pus (usaha) growing around an infected area.
tumour - a swelling caused by an abnormal growth of tissue. Can be serious (Malignant) au not serious (Benign).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…