Wana JF poleni na mihangaiko ya toka asubuhi.
Leo baada ya kutoka kanisani nilimkuta mama mmoja jirani yangu, akaniomba ushauri ila ilikuwa ngumu sana kwangu kumpatia jibu la moja kwa moja.
Mama aliniambia kuwa ametoroka na kila kitu kutoka kwa mumewe wa ndoa, ndoa yao walifunga kanisa la Anglikana.Yaani kabeba kila kitu, sababu ni kuwa wana ugomvi hawaelewani ndani ni mwaka mmoja sasa, hawaongei wala hakuna unyumba ingawa walikuwa wanaishi nyumba moja na kulala kitanda kimoja.
Sasa mama anauliza atafanyaje ili aweze kupata ela ya matumizi kwa ajili ya watoto?