Jirani yangu wa biashara amenisingizia kesi ya kutaka kumdhuru

man xule

Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
27
Reaction score
11
Wana JF naomba mchango wa maoni.
Mimi nikijana Nina miaka 28 kuna changamoto ninapitia na jirani yangu ninayefanyanae biashara inayo fanana katika eneo moja.

Tatizo kubwa ni kwamba mimi nikipata mteja yeye ananuna na akipata yeye mteja anafurahi huku akinipiga vijembe na ikitokea naongea na mteja wangu ananiangalia sana huku akidhani kwamba namzungumzia yeye.

Siku moja mungu akajalia nimepata wateja wengi Sana kuliko kawaida basi alinuna siku nzima mara ghafla ilipofika mida ya saa kumi na moja kafunga fremu yake huku akiongea mwenyewe ila nilipotezea sababu sijajua anaongelea nini ilipofika mida ya saa kumi na mbili nikamuona Kaka na police na kunitaka kufika kituoni nikakubali wito na baada ya kufika kituoni nikakuta ametoa maelezo ya kwamba amesikia nikiongea na mtu nikimwambia ya kwamba "UKIMUONA MALIZA".

Police alivyo muuliza kwamba umejuaje Kama ni wewe akasema amesikia nimemtaja jina lake Basi polisi wali niweka mahabusu baada ya muda ndugu wakaja niwekea dhamana na wakasema nitaitajika kurudi jumatatu.

Naombeni ushauri juu ya hili suala
 
Unaeza kwenda kufungua Case ya kudai fidia ni haki yako
 
Anafanya makusudi kukusumbua uhame hapo umuache mwenyewe
 
Anakutia jamba jamba ili uhame hapo hivyo wewe komaa na biashara mpaka atambue wewe ni mwamba.. pia case ya polisi komaa nayo mpaka akulipe fidia
 
Wana JF naomba mchango wa maoni.
Mimi nikijana Nina miaka 28 kuna changamoto ninapitia na jirani yangu ninayefanyanae biashara inayo fanana katika eneo moja.

Tatizo kubwa ni kwamba mimi nikipata mteja yeye ananuna na akipata yeye mteja anafurahi huku akinipiga vijembe na ikitokea naongea na mteja wangu ananiangalia sana huku akidhani kwamba namzungumzia yeye.

Siku moja mungu akajalia nimepata wateja wengi Sana kuliko kawaida basi alinuna siku nzima mara ghafla ilipofika mida ya saa kumi na moja kafunga fremu yake huku akiongea mwenyewe ila nilipotezea sababu sijajua anaongelea nini ilipofika mida ya saa kumi na mbili nikamuona Kaka na police na kunitaka kufika kituoni nikakubali wito na baada ya kufika kituoni nikakuta ametoa maelezo ya kwamba amesikia nikiongea na mtu nikimwambia ya kwamba "UKIMUONA MALIZA".

Police alivyo muuliza kwamba umejuaje Kama ni wewe akasema amesikia nimemtaja jina lake Basi polisi wali niweka mahabusu baada ya muda ndugu wakaja niwekea dhamana na wakasema nitaitajika kurudi jumatatu.

Naombeni ushauri juu ya hili suala
Wewe na jirani yako ni jinsia gani?

Na biashara yenu ni ya nini?
 
Back
Top Bottom