Wadau hope mko poa
Mimi nimehamia nyumba ya kupanga hivi karibuni. Nyumba hii inawapangaji wengi vijana wakike na wakiume.
Sasa mpangaji ambaye chumba changu kimetazana na chake ni binti mrembo sana. Ni binti ambaye toka siku ya kwanza nimefika kwenye hii nyumba amekuwa akinichangamkia sana. Mimi nafanya kazi naondoka asubuhi sana na huwa nachelewa mno kurudi. Ananijali sana katika vitu vya kawaida, mfano anaweza kuniletea chakula, kuna siku ananisaidia kujaza maji kwenye ndoo nk. Siku zingine huniambia amekuwa pekee na anahitaji kampani basi nitaenda kwake tutaangalia movie nk. Kiufupi anajihisi furaha akiwa karibu nami, ndivyo anavyiniambia.
Najua ana mtu wake na kuna siku huyu jamaa yake alikuja. Ni kwamba huyu binti alikosa ule uchangamfu kipindi jamaaa yake yupo
Sasa juzi kati hapa kanifungukia kuwa ananipenda sana na anatamani kila muda awe karibu na mimi sababu anaona mimi ni mwanaume nisiye na mambo mengi yaani tabia ya kuwa na wanawake ovyo sina. Nilivymuhujoji kuhusu jamaa yake akadai ni hampdndi anajilazimisha. Na pia akasema jamaa yake ni mwanajeshi hivyo muda mwingi huwa anaenda nje ya nchi na amesha sema waachana ila jamaa king'ang'anizi
Kiufupi demu ni mzuri sana, ila sasa mimi simuelewi kabisa hasa ukizingatia najua ana mtu. Sipendi kumuharibia jamaa. Nimefikiri kodi ikiisha nihame kimya kuepuka hili. Kingine wanaume ambao tuko mbali na wake na wapenzi wetu tuwe makini asee.
Niamue kipi, nipotezee na kuhama au niibomoe hii mali?