cha ajabu ni kwamba nchi jirani kama Rwanda, Burundi na pengine Uganda sina uhakika walimu wengi wanofundisha Lugha ya kiswahili ni Wakenya. je watanzania wenye Lugha sanifu tumeikalia hata kukosa walimu wa kiswahili nchi za nje? Nilikutana na mwalimu mmoja mjerumani kasoma kiswahili Tanzania na kiswahili chake sio kizuri lakini nafundisha lugha ya kiswahili kwenye chuo kimoja cha elimu Kigali.