Jisamehe kwa mambo mabaya uliyoyafanya

Jisamehe kwa mambo mabaya uliyoyafanya

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
FB_IMG_1725175449453.jpg

Ni Heri kidonda cha mguu kuliko cha moyo.

Watu wengi wanapitia mateso makali tena yanayochoma zaidi ya moto wa nyika na hii ni kutokana na kushindwa kusahau makosa waliyofanya kipindi cha nyuma. Hivyo, naomba andiko hili likakutoe kwenye gereza hilo kwa kujisamehe makosa yako.

Ni sawa kujisamehe makosa uliofanya, jisamehe kwa mawazo mabaya uliowahi kuwa nayo, jisamehe kwa maamuzi mabaya uliowahi kuchukua, jisamehe kwa watu wote uliowahi kuwaumiza, Jisamehe kwa fursa ulizo acha kwa sababu ya woga, jisamehe kwa kugombana na wazazi wako. Jisamehe kwa makosa uliyomfanyia mume au mkeo.

Usibebe makosa yaliyopita kwani yataendelea kuumiza moyo wako na kukukosesha furaha.
Yawezekana ulifanya wakati hujapata wakovu wa nafsi yako, hukuwa na ukomavu wa kiakili au ni ujana ulikusumbua. Na ulifanya makosa wakati hujapata uzoefu na ujasiri ulio nao sasa. Jisamehe sasa.
Jisamehe kwa maneno haya, “Ninajisamehe kwa makosa yangu yote ambayo niliwahi kufanya. Mimi ni mtu mwema. Ninaenda kuwa na baadae iliyo bora na nzuri”

Baada ya kujisamehe, sasa msamehe na mtakie baraka aliyekukosea, Mungu mbariki yeye. Namsamehe kwa kila kitu, na namtakia kila lililo jema maishani mwake.
Kama pia uliyemkosea unaweza kuomba msamaha aidha kwa ujumbe ama kuongea fanya hivyo na hata akikataa usiache kujisamehe.
 
Back
Top Bottom