Jitahidi Kuwa Mkweli

Jitahidi Kuwa Mkweli

Bwana Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2019
Posts
653
Reaction score
3,404
KUWA MKWELI SIKU ZOTE

Mwanamke aliingia kwenye bucha ya nyama na kuuliza
"Una kuku?"

Muuza nyama akafungua friza na kutoa kuku pekee ambaye ndiye alikuwa amesalia akamweka kwenye mizani. Mizani ikasoma Kilo 1.5.

Yule mwanamke akamtazama kuku kisha akauliza
"Hakuna mwingine ambaye walau ana kilo mbili?"

Muuza bucha akamrudisha kuku kwenye friza kisha akamtoa tena na kumuweka kwenye mizani. Kwa ujanja wa hali ya juu akakandamiza mizani kwa kidole gumba na mizani ikasoma kilo 2.

"Safi sana" Alisema yule mwanamke.
"Nitachukua kuku wote wawili"

Hadi sasa kichwa cha muuza nyama bado kipo ndani ya friza akitafuta kuku wa pili........


SEMA KWELI siku zote😂😂😂😂
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom