Sensei Tai
Senior Member
- May 26, 2022
- 168
- 466
Imekua ni kawaida kwa baadhi ya watu kufurahi pindi wanapoona mtu flani kaanguka iwe ni mtu mashuhuri au mtu wa kawaida ambae hana ushawishi wowote katika jamii, lakini pia kuna watu huwa wanasikitika kuona mtu flani kaanguka lakini hii inategemea ni kwa kiasi gani ulikua unaishi vizuri na jamii iliyokuzunguka.
Jana usiku niliona habari kwamba kuna viongozi wameondolewa kwenye nyadhfa zao lakini cha ajabu zaidi nilijaribu kupitia maoni tofauti tofauti ya wadau mbalimbali nikaona kwamba wengi wamefurahishwa zaidi na kuondolewa kiongozi flani kwenye nyadhfa yake kuliko hata wale wengine.
Akili ndo ikanijia kwamba huenda mtu yule alitumia vibaya cheo chake na kuona kwamba kwakua ana nafasi flani basi amemaliza haitaji kusikiliza watu wengine.
Sasa hali hii haipo tu kwa huyu kiongozi alieondolewa kwenye nafasi yake, hata mitaani na maofisini tupo na watu mbalimbali wa aina hii ambao wanaona kwakua wana cheo au nafasi flani basi hawana sababu ya kusikiliza wengine na wanajiona wao ndo wao utawaeleza nini.
Naamini kama uliishi vizuri na watu iwe ofisini kwako au hata mtaani kwako unapoishi siku ukianguka wengi watasikitika na huenda wakakusapoti ili urudi tena juu, lakini ukiona watu wanafurahia anguko lako basi yafaa ujitathmini mara mbili unakosea wapi.
Kuna watu leo hii wanawadharau wenzio kwasababu tu wana nafasi flani au wanafanya kazi sehemu flani na hata inapotokea misiba wanaangalia ni msiba gani wa kuhudhuria na je unaendana na hadhi yake.
Ndugu zangu yafaa tujitathmini sana mana hakuna aijuae kesho yake, yule alekufanya ukapata hiyo nafasi dakika sifuri tu anaweza kukutoa kwenye hiyo nafasi so jitahidi katika kipindi chote cha maisha yako kumuheshimu kila mtu awe na kitu au asiwe na kitu.