Jitihada za kuongeza mshahara Sekta Binafsi

Jitihada za kuongeza mshahara Sekta Binafsi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Katambi amesema serikali tayari imeunda bodi kwa ajili ya kufanya upembuzi ili kupata kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi.

"Tutarajie hivi karibuni tutakua tumepeta tangazo maalum la kazi walioifanya, kwa sababu wameshirikisha wadau wa sekta husika, hii imelenga kutatua changamoto katika sekta tofauti za binafsi" Katambi

Pia Katambi ameongeza kua "Hili linafanyika kwa kuangalia kiwango kilichopo cha sasa na kipya kulingana na kiwango cha uchumi na uhalisia wa maisha, kima cha mshahara kinachoendana na uhalisia"

Watanzania tunafurahi sana kunaona serikali ya Rais Samia Suluhu inavyowajali wananchi wake maana ni zaidi ya Watanzania milioni 1.5 wameajiriwa katika sekta binafsi.

Kwa miaka 9, waajiriwa wa sekta binafsi nchini hawajaongezewa mishahara. Serikali ya Rais Samia Suluhu inafanya mapitio ya kuongeza kima cha chini cha mishahara yao ili iendane na hali ya maisha.
 
Back
Top Bottom