Jitihada za Uhuru Kenyatta kurejesha amani Congo, ayataka makundi ya kigeni yenye silaha kurudi makwao

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Hotuba yake imenitia moyo.

Amenifurahisha alipozitaka nchi majirani kutoitumia ardhi ya Congo kama uwanja wa vita.

Kuna mapendekezo mengi ambayo yakifanyiwa kazi amani na ustawi utarejea Congo.

EeeeenHeeeee!

Kayataja hayo makundi bayana?

Utasubiri sana mkuu 'Joka Kuu'.
 
Jeuri na Ubabe wa Rais wa Rwanda ndio unataka kutia doa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki na Aftika kwa ujumla.

Matatizo kibao kwa wananchi wake halafu tena unaanzisha chokochoko!! huu ni ulevi wa madaraka!

lazima viongozi wetu waonywe waache huu upuuzi.
 
Binafsi ningependa zaidi kama Kenyatta angeitoa hiyo kauli akiwa bado ni Rais wa Kenya, naona ingekuwa na uzito unaostahili.

Lakini kuitoa sasa, sioni kama itakuwa na uzito stahiki kwasababu kama hii kauli isipompendeza Kagame, basi Ruto anaweza kuikana, aseme yale yalikuwa ni mawazo ya Kenyatta himself, na sio ya serikali yake.

Kwa mtindo huu, ndio maana bado naona Kagame ataendelea kuwa msumbufu wa eneo la ukanda huu wa maziwa makuu, ni kama vile marais wengine wa hili eneo wamemuacha atambe, ndio maana nae kila siku anakuja na kauli zake za kibabe na ujuaji.
 
Kwa kagame hiyo kauli haikubaliki, ameishasema yuko bize kuyarejeaha maeneo ya Rwanda yaliyomegwa i.e. (annexed na DRC)
 
..Hotuba yake imenitia moyo.

..Amenifurahisha alipozitaka nchi majirani kutoitumia ardhi ya Congo kama uwanja wa vita.

..kuna mapendekezo mengi ambayo yakifanyiwa kazi amani na ustawi utarejea Congo.

Hao Fdlr na Adf hayawezi kurudi kwao kirahisi hivyo bila maridhiano na nchi walizotoka ambazo hazitaki kabisa maridhiano nao....kumuambia Kagame awapokee Fdlr ni kutafuta ugomvi.

hata hao waliokubali amani huko Nairobi wape muda uone kama hawarudi msituni.
mtu chake zitto junior Moronight walker
 
Binafsi ningependa zaidi kama Kenyatta angeitoa hiyo kauli akiwa bado ni Rais wa Kenya, naona ingekuwa na uzito unaostahili.

Lakini kuitoa sasa, sioni kama itakuwa na uzito stahiki kwasababu kama hii kauli isipompendeza Kagame, basi Ruto anaweza kuikana, aseme yale yalikuwa ni mawazo ya Kenyatta himself, na sio ya serikali yake.

Kwa mtindo huu, ndio maana bado naona Kagame ataendelea kuwa msumbufu wa eneo la ukanda huu wa maziwa makuu, ni kama vile marais wengine wa hili eneo wamemuacha atambe, ndio maana nae kila siku anakuja na kauli zake za kibabe na ujuaji.
Aogopwe vipi wakati Kenya na baadhi ya mataifa yamepeleka vikosi kupambana na M23 wanaofadhiliwa na Rwanda.

Na hata Rais wa Congo DR amemtaja waziwazi Kagame aache mara moja kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyoua raia wa Congo kwa lengo la kufanya uporaji.

Pia Rais mstaafu Kikwete alipeleka jeshi letu kupambana na hao magaidi ya Kagame huku akimuonya Kagame kuacha kuiyumbisha jumuia kwa maslahi yake binafsi.
 
M23 ni Jeshi la Rwanda, limevamia CongoDR, ndio maana wakitaka kupewa kichapo, wanajeshi wenzao wa Rwanda wanajifanya kuwatetea. Jiwe ndio alivuruga mpango mzima uliowaondoa M23 Congo, wakarudi kwao Rwanda. Jiwe akajiunga na kagame, the whole process ikarudi nyuma.
 
Back
Top Bottom