Katika hali ya kawaida ukimuuliza Mtanzania unajivunia nini katika nchi yako, atakutajia vivutio vya utalii kama Serengeti, Ngorongoro au mlima Kilimanjaro. Anaweza kwenda mbali zaidi na kutaja adhina kama madini na gesi. Vile vile ukimuuliza mdada nini anajivunia si ajabu akakuelezea vile muonekano wake kiumbo na kisura jinsi unavyowapagawisha wanaume. Usishangae pia ukupata majibu ya namna hiyo kutoka kwa vijana wa kiume kwa kizazi cha sasa.
Majibu hayo si mabaya, lakini ni wazi kuwa sifa hizo ni asilia, hivyo hatuna mchango wowote katika upatikanaji wake. Kiasi fulani sifa za aina hii zinatudumaza, tunaona kwamba sisi ni taifa teule na vile tulivyobarikiwa inatosha kutambulika kwa sifa hizo. Hatutumii fursa za kuwa na sifa hizo kutupatia maendeleo, ambayo pia yatakua ni sifa zetu. Kuwa na mlima Kilimanjaro na mbuga za Serengeti na Ngorongoro tu haitoshi, je uwepo wa vivutio hivi umechangia vipi mabadiliko chanya ya wamiliki wake ambao ni Watanzania? Je tumeongeza sifa ya kuwa nchi inayoongoza kutembelewa zaidi Africa?
Ukichunguza nchi nyingi zilizoendelea sifa zao ni matokeo ya yale waliyoyafanya kwa kutumia rasilimali walizonazo, au hata walizopora. Mji wa Dubai mathalani ni moja ya miji inayoongoza kutembelewa zaidi duniani na sababu kubwa ni za kibiashara au kiutalii. Sifa hii imetokana na juhudi binafsi za kuendeleza mji wao ambao hapo awali ulikua kama jangwa. Leo hii wameweza kutuzidi Sisi katika sekta ya utalii, ambapo kiuhalisia tuna vivutio vingi asilia kuliko wao.
Pengine Dubai ni mbali sana lakini vipi kuhusu mji wa Kigali, Rwanda hapa hapa Afrika ya Mashariki. Kwa miaka kadhaa umekua ukiongoza kama mji wa kwanza kwa usafi katika mataifa yote ya Afrika ya Mashariki, wamefika mbali zaidi katika kuutangaza utalii wa nchi yao katika mambo ambayo wameyatolea jasho wenyewe.
Sasa ivi kampeni ya "Visit Rwanda" inatangazwa na vilabu vikubwa kama Arsenal na Psg. Ambapo kiuhalisia utazamaji wa watu kwa mechi moja uwanjani si chini wastani wa watu 50,000 bila Kujumuisha mamilioni ya watu wanaotazama kupitia runinga na mitandao. Unaweza kuona jinsi mikakati yao ilivyo na ufanisi, na si ajabu baada ya miaka kadhaa wakaongoza kutembelewa zaidi mbele ya sisi tunaojisifu kuwa tuna vivutio vingi bila kufanya mikakati madhubuti kufika mbali zaidi.
Ni wazi Kwamba serikali inatakiwa iweke mikakati madhubuti katika kuhakikisha sifa hizi zinamfaidisha Mtanzania, kuleta maendeleo yatakayoliongezea sifa zaidi taifa hili. Hakutakua na maana kama Tanzanite inapatikana Tanzania pekee lakini wauzaji wake wakubwa wawe ni wa Africa Kusini, Au Serengeti ni mbuga yenye vivutio zaidi lakini watalii wengi wanatembele Maasai Mara, Kenya .
Ukiichana na mambo ya Kiserikali, hali ya kuridhika kwa vitu ambavyo hatujavitolea jasho yanadudumiza maendeleo yetu binafsi. Habari ya kujisifia vile umeumbwa inapelekea kuwa na wadangaji wengi ambao wanaona muonekano wao ni ajira tosha, na wanapaswa kulipwa iwe ni kwenye mahusiano au biashara binafsi. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama tabia hizi zitafanywa na watoto wa kiume. Unaweza kufanya chunguzi binafsi kuona jinsi watoto wa kiume wanaojali muonekano wao kuliko kazi vile walivyopotoka kimaadili, mpaka kufikia hatua za kukiuka mila na desturi za mtanzania.
Andiko hili halitakua na maana kama halitotoa mapendekezo ya nini kifanyike kuachanana na desturi hii inayotududumiza bila kujua.
Kutumia watu wenye ushawishi zaidi nje ya Tanzania kama mabalozi wa utalii. Kwa kua lengo letu ni kuwavutia zaidi watu walio nje ya Tanzania au Afrika kututembelea, itakua rahisi zaidi kwa walengwa kumuelewa mtu wao zaidi kuliko mtu wetu. Pata picha mchezaji kama Kylian Mbape anakuja kutumia likizo yake Tanzania na anarusha picha zake kwenye mitandao yake ya kijamii kuonyesha vile amevutiwa na safari yake. Matokeo ya ushawishi wake yatakua makubwa kwa wachezaji wenzake na watu wanaomfuatilia. Tukiendelea kutumia washawishi wa ndani, tutakua kama tunajitekenya wenyewe na sina uhakika kama tutacheka au la.
Kuvutia watalii ni jambo la kwanza, kinachofuata ni kuhakikisha kilichopatikana kutokana na ujio wao kinamnufaisha Mtanzania moja kwa moja. Hapa serikali unahusika kwa asilimia mia. Kwa kipindi kirefu faida izi zimekua zikiwaendea watu wachache walafi na wabinafsi wa rasilimali za Tanzania. Ifike muda sasa hatua zichukuliwe kudhibiti watumishi wa haiba hii.
Kijamii taasisi zinatakiwa zitoe elimu kwa vijana na watoto mathalani kuhusu vile heshima na sifa ya mtu huja kutokana na vile alivyovifanya katika jamii husika na sio muonekano. Na taasisi ya kwanza hapa ni familia kwa sababu ndio ina ukaribu zaidi na watoto na vijana kuliko taasisi nyingine. Tukifanya hivi tutawajengea misingi bora ya uchapakazi hata watakapokuja kupata nafasi mbali mbali za kutumikia jamii, watasimama katika misingi waliyokuzwa.
Ni vema tukakumbushana katika kizazi hiki, maendeleo ya sayansi na teknolojia yameambatana na matokeo mengi hasi katika makuzi ya vijana. Uvivu, biashara za ngono, mapenzi ya jinsia moja na matumizi ya mihadarati ni baadhi ya matokeo hayo. Hivyo unapopata nafasi ya kuelimisha au kumsaidia mtu yeyote kuondokana na janga hilo, tafadhali fanya hivyo bila kujali mahusiano au itikadi zozote zinazoweza kuwatofautisha.

Upvote
1