Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kiti hiki ndicho alichoketi Bi. Elizabeth II wakati anatawazwa kuwa Malkia wa Uingereza mnamo mwaka 1953. Kimetumika kutawazia wafalme na malkia waliotawala dola ya uingereza tangu mwaka 1300. Kinaitwa kiti cha mfalme Edward "King Edward's Chair".
Ukiangalia vizuri hapo kitini, utaona kuna jiwe. Historia ya jiwe hilo inaturudisha mwaka 1296 kulipozuka vita kati ya Uingereza na Uskochi 'Scotland' ambapo majeshi ya uingereza chini ya mfalme Edward yalivamia uskochi na kunyang'anya jiwe hilo. Ni jiwe lililotumika kama kiti, ambacho wafalme wa uskochi hukalia wakati wa kutawazwa.
Ndipo likachukuliwa hadi uingereza na kubebezwa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mbao ili kitumike kwa shughuli maalumu ya kutawazwa kwa mfalme. Hiyo ni alama kwamba wafalme wa Uingereza ndio sasa wanakuwa watawala wa Scotland.
Ni miaka 722 sasa. Watu ishirini na sita (26) wamevikwa taji katika kiti hiko. Mara ya mwisho kutumika ni mwaka 1953 wakati wa kumtawaza malkia Elizabeth II.
Wakati wa kutawazwa mfalme/malkia wa Uingereza, huwa kuna wimbo maalumu 'anthem' huimbwa. Wimbo huo huitwa "Zadok the Priest" au kwa kiswahili 'Kuhani Sadoki'. Wimbo huu umeanza kutumika mwaka 1727 katika kutawazwa mfalme George II.
Maudhui na maneno ya wimbo huo yametokana na tukio la kutawazwa kwa mfalme Selemani wa Israel. Ukisoma biblia kitabu cha 1 wafalme 1:38-40, utaona wakati kuhani Sadoki anamtawaza Solomoni kuwa mfalme, wananchi walishangilia na kuimba kwa sauti wakisema "Aishi Mfalme", "Aishi Mfalme Solomon". "Live long the King".
Hata wimbo wa taifa wa Uingereza "God Save the Queen" umebeba maudhui na maneno yasemayo "live long the queen" yaani 'aishi muda mrefu malkia'.
Katika biblia kuna habari ya mtu aliyeitwa Yakobo. Siku moja aliondoka Beer-sheba, akaelekea Harani. Alipofika mahali fulani, akalala hapo kwa sababu jua lilikuwa limetua. Alichukua jiwe moja la mahali hapo, akaliweka chini ya kichwa chake, akalala.
Aliota ndoto, na katika ndoto hiyo, aliona ngazi iliyosimamishwa duniani na ncha yake inafika mbinguni. Malaika wa Mungu walikuwa wakipanda na kushuka katika ngazi hiyo. Mwenyezi-Mungu alisimama juu ya ngazi hiyo, akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi unayoilalia nitakupa wewe na wazawa wako".
Yakobo alipoamka usingizini, akasema, “Hakika, Mwenyezi-Mungu yupo mahali hapa. Akaogopa na kusema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ni nyumba ya Mungu na lango la mbinguni.”
Kisha Yakobo akachukua lile jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimika kama nguzo na kuliweka wakfu kwa kulimiminia mafuta. Akapaita mahali hapo Betheli. Habari hiyo inapatikana Kitabu cha Mwanzo 28:10.
Sasa, inavyosemekana ni kwamba, hilo jiwe lilikuja kuchukuliwa na kufikishwa Scotland. Na ndio hilo likawa linatumika kutawazia wafalme wa uskochi kabla ya kutwaliwa na Uingereza mwaka 1296.
Hata hivyo, mwaka 1996 serikali ya Uingereza iliamua kulirudisha nchini Scotland. Kwahiyo 'kiti cha king Edward' kimebaki bila jiwe. Huenda Mfalme ajaye atakalia kiti kisicho na jiwe.
Wakatabahu;
©KichwaKikuu.