SoC02 Jiwe La Msingi 1. Ukombozi wa Fikra, Uchumi na Elimu

SoC02 Jiwe La Msingi 1. Ukombozi wa Fikra, Uchumi na Elimu

Stories of Change - 2022 Competition

onea 22

Member
Joined
Jul 31, 2020
Posts
34
Reaction score
20
UTANGULIZI

PAMOJA na uwezo mkubwa alionao mwanadamu wa kutatua changamoto mbalimbali katika mazingira yanayomzunguka, Watanzania wameshindwa kutatua changamoto za msingi ambazo ndiyo msingi mkuu wa maisha ya mwanadamu ulimwenguni.

Si Watanzania wote wenye uwezo wa kutafakari na kuwaza nini kilichotupelekea Watanzania wengi kuwa katika hali tuliyo nayo sasa kiuchumi na kijamii. Wengi wetu tumekuwa watumwa wa mifumo ambayo kimsingi imeonekana kushindwa kufanya kazi si kwa Tanzania tu, bali hata katika nchi nyingine karibu zote za dunia ya tatu.

Mifumo hiyo ya wanaadamu pamoja na hekaheka zake za kutaka kurahisisha maisha zimepelekea mrundikano wa changamoto nyingi zaidi kwao wenyewe na viumbe vingine vilivyomo duniani.

Kwa mfano tunapoharibu safu ya ozone (ozone layer) mwathirika wa moja kwa moja si mwanadamu pekee, ila hata viumbe vingine vinavyotegemea mwanga wa jua wa wastani. Mfano mwingine lilipopigwa kombora la nyuklia kule Heroshima si watu tu wa Japani walioathirika, kuna viumbe wengine wengi tu waliopoteza maisha na kuharibiwa mfumo mzima na utaratibu wa maisha yao.

Binadamu wachache hasa wa dunia ya kwanza waliopewa (waliojipa) dhamana ya kufanya mwanadamu aendelee kuwapo kwa muda mrefu kwenye uso wa dunia, wametumia mwanya huo kuwakandamiza walio wengi na kuwawekea mifumo ya kuwafanya wajione wao ni wajinga wasioweza kufanya jambo lolote bila msaada kutoka nje.

Jambo ambalo si kwamba tu sio kweli bali ndio mtego wa kuwafanya walio wengi washindwe kujinasua kwenye changamoto mbalimbali zinazowakabili. Kwa nchi za dunia ya tatu mfano huu ni sawa na ule wa mtu aliyetekwa na majambazi, akafungwa kamba mwili mzima kisha kwa manufaa ya hao majambazi wakaona wasimuue bali wamuache wamemfunga ili wamtumie vizuri.

Yule mtu akatamani kuwa huru lakini mipango yake yote ya kukata kamba na kutoroka akawa anawashirikisha wale majambazi na wakati mwingine kuwaomba ushauri kabisa afanye nini ili aweze kujifungua hizo kamba? bila shaka ataendelea kukaa milele akiwa amefungwa hadi pale atakapobadili fikra zake.

Kiuhalisia adui yake namba moja ni yeye mwenyewe kwani anavujisha mbinu za kujinasua kutoka kwenye janga kwa adui zake. Siku atakayoacha kujisaliti ndio itakuwa mwanzo wa uhuru wake.

Mgawanyo Wa Jamii Ya Watanzania Kwa Mujibu Wa Shughuli Zao Za Kiuchumi.

Kwa kutumia kigezo cha shughuli za kijiingizia kipato za wananchi, jamii ya Watanzania inaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo



Serikali

Hiki ni kikundi cha watu ambao wanapanga mustakabali mzima wa jamii ya watanzania. Kundi hili la Watanzania linajumuisha watu wa Serikali kuu, mahakama na bunge. Kundi hili la watanzania kwa asilimia kubwa halina changamoto za kiuchumi.

(b)Wafanyakazi Wa Umma

Hawa ni kundi la watu ambao wanafanya kazi chini ya serikali. Mwajiri wao mkuu ni serikali lakini hufanya kazi kwa manufaa ya jamii nzima ya Watanzania. Mfano wa wanaoingia katika kundi hili ni pamoja na walimu, wauguzi, madaktari na watumishi wengine wa fani tofauti. Kundi hili la Watanzania wamegawanyika mara mbili, kuna ambao wanaishi maisha mazuri lakini wengine bado wana changamoto za maisha kutokana na uelewa na mikakati ya mtu husika.

(c)Wafanyabiashara Wakubwa

Katika kundi hili wanaingia wamiliki wa viwanda vikubwa na vidogo, wamiliki wa biashara za usafirishaji n.k . Pamoja na Watanzania weusi katika kundi hili wengi wao ni Watanzania wenye asili ya Asia. Kundi hili halina changamoto kubwa sana kwenye namna ya kuendesha maisha yao na kupata mahitaji yao ya muhimu ya kila siku.

(d) Wafanyakazi wa Viwandani

Watu hawa wanafanya kazi chini ya wafanyabiashara wakubwa. Wengi wao hufanya kazi kama vibarua kwa ujira mdogo sana. Ni nadra sana kukuta wafanyakazi wa viwandani wakipokea hata 200,000 tsh/= kwa mwezi (kwa mwaka 2017). Maisha ya watu hawa ni yale ambayo waswahili wanasema maisha ya kijungu jiko. Kwa maana ya kwamba wanachokipata kinaishia kwenye chakula na kulipa pango ya chumba tu.

(e) Watu wa janjajanja

Kundi hili la Watanzania linajumuisha watu kutoka katika makundi mengine karibu yote. Hawa na Watanzania ambao wanaendesha maisha yao/wamefanikiwa kimaisha kwa njia ya kuwaaminisha watu vitu ambavyo mara nyingi huwa si vya kweli. Humu wanaingia viongozi wa dini, Madaktari (hasa wa tiba mbadala), wanasiasa n.k.

(f) Wajasiliamali

Sehemu hii inaingia kundi kubwa la Watanzania. Ujasiliamali kwa Tanzania unaweza kugawanyika katika makundi mawili pia. Makundi hayo ni pamoja na

(i) Wakulima na wafugaji

Hili ndio kundi la wazalishaji wakuu katika jamii ya Watanzania. Zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo. Maisha ya kundi hili la Watanzania ni duni sana, na katika shughuli zao wanatumia zana duni zilizopitwa na wakati.

(ii) Walanguzi

Hawa ni watu wa kati ambao wanarahisiha upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa jamii. Mara nyingi huwa hawazalishi bidhaa yoyote, bali wao wananunua kutoka kwa wakulima na wafugaji kasha kwenda kuviuza tena mijini.

(g) Watu Tegemezi

Hili ni kundi la watu ambao wanaitegemea jamii ili waweze kuishi. Katika kundi hili wanaingia watoto wadogo, wazee, walemavu. Watu tajwa hapo juu wanakidhi vigezo vya kuingia kwenye kundi hili. Lakini pia katika kundi hili wanaingia vijana ambao hawana kazi majumbani, vibaka , wezi na hata wadada wanaojiuza mabarabarani.



Changamoto Zinazoikabili Jamii ya Watanzania.

Je, jamii ya Watanzania inakabiliwa na changamoto zipi?

Ili kuzifahamu kwa urahisi itatubidi kuyatupia macho malengo ya maendeleo ya millennia (MDG’s) ambayo baadaye (2016) ili kuonyesha kuthamini maisha ya viumbe wajao yalibadilishwa jina na kuwa Sustainable Development Goals (SDG’s).

Malengo ambayo yaliwekwa ni pamoja na;

1. Kutokomeza ufukara/umasikini uliopindukia na njaa.

2. Kutoa elimu ya msingi kwa watu wote.

3. Kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.

4. Kupunguza vifo vya watoto wachanga.

5. Kuboresha afya za wazazi wa kike.

6. Kupambana na UKIMWI, Malaria na magonjwa mengine.

7. Kuboresha mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo vya mwanadamu na viumbe vingine.

8. Kuanzisha ushirikiano wa kidunia kwa ajili ya maendeleo.

Hizo ni baadhi tu ya changamoto ambazo zinawakabili Watanzania na jamii nzima ya dunia ya tatu kwa jumla.

Ni jukumu la kila Mtanzania kuangalia kwa makini changamoto hizo (SDGs) na nyingine nyingi ambazo hazijaainishwa hapo juu na kujaribu kuzitafutia suluhu na si kuwaachia watu wa dunia ya kwanza kutufanyia kila kitu.

Kutokana na masharti ya 2022 story of change challange, sitaweza kuandika zaidi ya maneno 1000. Ila nitaandika nyuzi nyingine ili kuweza kukamilisha mawazo nayotaka kushare nanyi.

Maulid Siogopi
0753887199.
 
Upvote 1
Nimependa hii ya watu wajanjawajanja. Tanzania Hawa ni wengi mno.
 
na kwa dunia jinsi watu walivyo siriazi na mambo yao!!!itatuchukua muda mrefu sanaa kufika nchi ya ahadi..
Ni kweli kabisa. Safari ni ndefu bado. Lakini kupitia maandiko haya, tutazidi kuleta fikra chanya.
 
Back
Top Bottom